Raila Odinga akana kuitisha maandamano siku ya uchaguzi

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amewataka wafuasi wake kutoandamana na badala yake kusalia majumbani mwao siku ya uchaguzi.
Maelezo ya picha,

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amewataka wafuasi wake kutoandamana na badala yake kusalia majumbani mwao siku ya uchaguzi.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amewataka wafuasi wake kutoandamana na badala yake kusalia majumbani mwao siku ya uchaguzi.

''Hatujawaambia watu wafanye maandamano siku ya uchaguzi. Hatujasema hilo hata kidogo'', Odinga alisema siku ya Jumanne katika mahojiano na BBC.

Alhamisi iliopita , Bwana Odinga na upinzani wake wa Nasa uliwaambia wafuasi wao kujiandaa kufanya maandamano wiki ya Uchaguzi mkuu.

Lakini katika mahojiano, bwana Odinga alisema kuwa maoni yake ni tofauti na yale ya rais Uhuru Kenyatta ambaye amesisitiza kwamba ni lazima uchaguzi ufanyike katika kipindi cha siku 60 kama ilivyoagizwa na mahakama ya juu.

''Kuna kambi mbili hapa, wale ambao wanataka kushiriki katika uchaguzi usio huru na haki na wale ambao wanasema hapana sio sawa kufanya hivyo'', alisema Odinga.

Maelezo ya picha,

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Baada ya Raila Odinga kushinda katika malalamishi yake aliyoiwasilisha mahakamani , tume ya uchaguzi ilichapisha tarahe 26 kuwa tarahe ya uchaguzi mpya baada ya mahakama ya juu kufutilia mbali ushindi wa rais Uhuru Kenyatta.

Lakini bwana Odinga aliwasilisha orodha ya masharti kwa tume ya uchaguzi ambayo alisema ni sharti yaafikiwe kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mpya ikiwemo kubadilishwa kwa kampuni itakayochapisha makaratasi ya kupigia kura, kampuni yenye mfumo wa kielektroniki ya kupigia kura, mbali na kushinikizwa kujiuzulu kwa afisa mkuu wa tume hiyo Ezra Chiloba pamoja na maafisa wengine wakuu wa tujme hiyo.

Wiki mbili kabla ya uchaguzi , bwana Odinga alijiondoa katika uchaguzi huo na kutaka uchaguzi mpya kufanyika baada ya siku 90 baada ya uteuzi kufanywa.

Lakini uamuzi wa mahakama kuu uliowaruhusu wagombea wengine wanane kushiriki katika uchaguzi huo ulimrudisha rais Odinga katika wagombea wanaofaa kushiriki katika uchaguzi, huku rais Uhuru Kenyatta akisema kuwa ni chaguo la Odinga kushiriki uchaguzi huo au la.

Katika mahojiano hayo bwana Odinga amelitaja kama jaribio la kuwatishia Wakenya hatua ya vigogo wa chama tawala cha Jubilee kuvalia magwanda ya kijeshi.