Mwanamfalme aapa kurudisha 'Uislamu wa wastani' Saudia

Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman

Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman amesema kuwa kurudishwa kwa Uislamu wa kadri ni muhimu katika mipango yake kuufanya ufalme huo wa Ghuba kuwa wa kisasa.

Aliwaambia maripota kwamba asilimia 70 ya idadi ya raia wa Saudia wana umri wa chini ya miaka 30 na kwamba wanahitaji maisha ambapo dini itataka watu kuvumiliana.

Mwanamfalme huyo ameapa kuondoa itikadi kali hivi karibuni.

Alitoa matamshi hayo baada ya kutangaza uwekezaji wa $500 katika mji mpya wa kibiashara.

Kwa jina NEOM, mji huo utajengwa kilomita 26,500 kaskazini mwa Saudia katika pwani ya bahari ya shamu karibu na Misri na Jordan.

Familia ya kifalme ya Saudia na imani ya kidini wanafuata madhehebu ya Sunni kwa jina Wahhabi na Mfalme anajichukulia kuwa mlinzi wa maeneo mawili ya Kiislamu yalio takatifu.

Sheria za kiislamu na mavazi yake yanaheshimika pakubwa katika ufalme huo.

Mwaka uliopita , mwanamfalme Mohammed alitoa mipango kadhaa ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kwa ufalme huo unaotumia utajiri wa mafuta unaojulikana kama maono ya 2020.

Ikiwa miongoni mwa mabadiliko, Mohammed mwenye umri wa miaka 32 amependekeza ubinafsishaji wa kampuni ya mafuta Saudi Aramco mbali na kuanzisha wakfu mkubwa zaidi.