West Ham yailaza Spurs na kutinga robo fainali ya Carabao

Andre Ayew baada ya kuifungia West Ham bao Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Andre Ayew aliifungia West Ham mabao mawili

Hii ni baada ya West Ham kumudu kujikwamua kutoka mabao mawili chini na kumaliza kwa kuifunga Tottenham Spurs mabao matatu kwa hayo yao mawili .Na kwa ushindi huo West Ham sasa imefuzu robo fainali kombe la Carabao..

Andre Ayew raia wa Ghana ndiye aliyefunga mabao mawili ya mechi hiyo huku Angelo Ogbonna akiongeza la tatu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Slaven Bilic amekwisha shinda mabao 42 katika mechi zake 109 kama meneja wa West Ham

Tottenham Spurs ilikuwa imeanza mechi hiyo kwa kishindo pale walipofunga bao la kwanza kwenye dadika 5 tu za mechi hiyo iliyochezwa huko Wembley.

Mpangilio wa timu na mechi za duru inayofuata ya mchuano huo unatangazwa baadae leo.