Abiria asafiri katika ndege akiwa pekee

Alihudumiwa kama mtu muhimu sana VIP baada ya abiria wawili waliotarajiwa kuabiri ndege hiyo kukosa kufanya hivyo.
Image caption Alihudumiwa kama mtu muhimu sana VIP baada ya abiria wawili waliotarajiwa kuabiri ndege hiyo kukosa kufanya hivyo.

Mwanamke aliyelipa nauli ya ndege ya £46 kuelekea Crete ameshangazwa baada ya kujipata kuwa abiria wa pekee katika ndege.

Karon Grieve kutoka Dunlop mjini Ayrshire aliitaja ndege hiyo aina ya Jet2 inayosafiri kutoka Glasgow hadi kisiwa cha Ugiriki ambayo kwa kawaida huwabeba abiria 189 kuwa ya kushangaza.

Alihudumiwa kama mtu muhimu sana VIP baada ya abiria wawili waliotarajiwa kuabiri ndege hiyo kukosa kufanya hivyo.

Jet2 ilisema kuwa sio jambo la kawaida kwa ndege ya mwisho ya msimu kuwa na abiria wachache.

Bi Grieve aliyekuwa akisafiri kuelekea Crete ili kuandika riwaya alisema kuwa ilikuwa wazi kwamba kulikuwa na abiria wachache wakati alipowasili katika uwanja wa ndege ili kuabiri ndege hiyo siku Jumapili.

Aliambia BBC kwamba: Niliwasili katika eneo la kukaguliwa na kwa mzaha nikawauliza wafanyikazi wa ndege , ni watu wangapi waliabiri ndege hiyo.

Tulianza na watu 10 hadi kufikia watu wanne na akasema huwezi kudhania kuna watu watatu pekee.

Lakini nilipoingia katika lango la mwisho la kwenda kuabiri ndege , watu wengine wawili hawakujitokeza.

Image caption Bi Grieve alisema kuwa alipanga kusalia mjini Crete kwa mwezi mmoja akiandika kitabu chake kabla ya kurudi Uskochi.

Bi Grieve alisema kwa kuwa yeye ni abiria wa pekee wafanyikazi wote wa ndege hiyo walikuwa wakilijua jina lake.

Alisema: Tulikuwa marafiki wakubwa hata kabla ya mimi kuingia katika ndege.Rubani wa ndege alikuwa mzuri.

Baada ya ndege kupaa angani bi Griev aliniita kwa jina langu akiwa katika chumba cha urubani.

Alisema hujambo Karon, utaona Croatia upande wako wa kushoto na tutasafiri katikati ya kimbunga hiki na baadaye alikuja na kusema.

Tafadhalini Karon na wafanyikazi jaribuni kwenda upande mwengine wa ndege na mutazame ''ni kitu cha kushangaza''.

Bi Grieve alisema kuwa alipanga kusalia mjini Crete kwa mwezi mmoja akiandika kitabu chake kabla ya kurudi Uskochi.

Hatahivyo amesema ni vigumu kujipata katika hali kama hiyo atakaropejea Uskochi.

Mada zinazohusiana