Kwa Picha: Uchaguzi wa marudio Kenya 26 Oktoba

Uchaguzi wa urais wa marudio ulifanyika nchini Kenya leo ambapo idadi ya waliojitokeza kushiriki ilikuwa chini ukilinganisha na uchaguzi wa tarehe 8 Agosti.

Kawira
Image caption Bi Kawira Mugo akionesha wino kwenye kidole chake baada ya kupiga kura katika kituo cha MP Patel mjini Eldoret magharibi mwa Kenya.

Mgombea wa upinzani Raila Odinga alisusia na alikuwa amewahimiza wafuasi wake kususia.

Ingawa upigaji kura uliendelea vyema ngome za serikali, katika ngome za upinzani uchaguzi ulitatizika kutokana na maandamano na makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa Bw Odinga.

Uchaguzi katika majimbo manne umeahirishwa hadi Jumamosi na tume ya uchaguzi.

Huu hapa ni mseto wa picha za hali ilivyokuwa maeneo mbalimbali nchini humo.

Tuanze na mwanamume huyu katika eneo la Katwekera katika mtaa wa Kibera, Nairobi ambaye alijipata amezingirwa na maafisa wa polisi.

Polisi wakikabili mwandamanaji Katwekera, Kibera Haki miliki ya picha AFP/Getty

Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya waandamanaji. Mwanamume huyu alirushiwa bomu la kutoa machozi Kibera.

Kukwepa bomu la machozi Haki miliki ya picha AFP/Getty
Mwandamanaji Kibera Haki miliki ya picha AFP/Getty

Hapa chini ni masanduku ya kupigia kura ya eneo bunge la Kisumu ya Kati ambayo hayakusafirishwa vituoni. Eneo hilo lina vituo 196.

Masanduku ya kura Haki miliki ya picha AFP/Getty

Mjini Kajiado, hali ilikuwa tulivu. Mwanamke huyu anaonekana akipakwa wino kwenye kidole chake baada ya kupiga kura yake.

Kajiado Haki miliki ya picha AFP/Getty

Familia hii ilifika katika kituo cha kupigia kura cha Mutomo, Gatundu katika jimbo la Kiambu na mavazi ya kipekee - mavazi ya rangi za bendera ya Kenya.

Mavazi ya bendera

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitimiza miaka 56 hivi leo. Alizaliwa siku sawa na ya leo mwaka 1961.Watoto hawa wamekuwa kwenye kituo cha kupigia kura cha Mutomo, ambacho ndicho Bw Kenyatta, wakiwa na fulana zenye ujumbe wa kumtakia heri siku ya kuzaliwa kwake.

Maua Mutomo

Rais Uhuru Kenyatta baada ya kupiga kura katika kituo cha Mutomo, Gatundu katika jimbo la Kiambu alisema wakati umefika kwa taifa hilo kusonga mbele. Hapa anaonekana akipiga picha ya selfie na mmoja wa waliokuwa kituoni.

Uhuru Kenyatta na mpiga kura - 26 October 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Uhuru Kenyatta baada ya kupiga kura alisema wakati umefika kwa taifa hilo kusonga mbele

Katika kituo hicho cha Mutomo, kulikuwa na mbwa huyu langoni. Alitaka kupiga kura pia?

Mbwa Mutomo Haki miliki ya picha AFP/Getty

Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea na matokeo yanatarajiwa kutangazwa katika kipindi cha siku saba.

Hapa ni shughuli ya kuhesabu kura katika kituo kimoja Kisumu.

Kuhesabiwa kwa kura Mombasa Haki miliki ya picha AFP/Getty

Picha kwa hisani ya AFP, Getty Images, BBC