Mtu aliyelipwa kuua watu akamatwa baada ya vifo vya watu 70 Pakistan

Alleged contract killer in courtroom Haki miliki ya picha Magyar Televizio
Image caption TV ya Hungary ilimuonyesha mtu huyo

Mwanamume mmoja raia wa Pakistan ambaye amekuwa akitafutwa na polisi wa kimataifa wa Interpol kwa madai kuwa alilipwa kuua watu, amekamatwa nchini Hungary.

Mamlaka nchini Pakistan zilikuwa zimetangaza waranti wa kimataifa wa kumkamata mtu huyo kutokana na vifo 70 nchini humo, na kumuorodhesha kuwa mtu aliyekuwa akitafuwa zaidi nchini Pakistan.

Polisi walisema kuwa alikamatwa akiwa miongoni mwa wahamiaji waliokuwa wakisafirishwa kiharamu kwenda Ausralia.

Mtu huyo wa umri wa miaka 35 anatajwa kufahamika kama "Mchinjaji MPakistan.

Kundi alilokuwa akisafiri nalo lizuiwa eneo la Boly, kilomita 175 kusini mwa mji wa Budapest.

Boly uko karibu na mpaka wa Hungary karibu na Croatia na Serbia.

Kusafirishwa kwake kwenda Pakistan kutaamuliwa siku zinazokuja.

"Kisa hiki kinaashiria umuhimu uliopo kwenye ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na uhalifu," waziri wa mambo ya ndani wa Autralia alisema.