Burundi yajiondoa rasmi katika mahakama ya ICC

Rais Nkurunziza alichukua madaraka kwa awamu ya tatu, licha ya kuwepo kwa kipindi cha mihula miwili katika katiba ya taifa hilo.
Image caption Rais Nkurunziza alichukua madaraka kwa awamu ya tatu, licha ya kuwepo kwa kipindi cha mihula miwili katika katiba ya taifa hilo.

Burundi limekuwa taifa la kwanza mwanachama wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa jinai kujiondoa katika mahakama hiyo.

Serikali ya taifa hilo la Afrika ya kati liliuarifu Umoja wa Mataifa UN kuhusu hatua hiyo mwaka mmmoja uliopita , na hii leo kujitoa kwao kunaanza kuidhinishwa rasmi.

Inaonekana kama kipimo cha jamii ya kimataifa kuhusu haki.

Ni hatua sio ya kawaida.

Je kutakuwa na athari zake na ni kwa nini ni muhimu?.

Kulingana na mwandishi wa BBC Anna Holligan kujiondoa kwa Burundi ni majuto makubwa.

Mahakama ya ICC imeanza kutathmini iwapo inaweza kuchunguza ghasia za kisiasa zilizoibuka baada ya rais Nkurunziza kuchukuwa madaraka kwa awamu ya tatu, licha ya kuwepo kwa kipindi cha mihula miwili katika katiba ya taifa hilo.

Image caption Makao makuu ya mahakama ya ICC mjini Hague

ICC bado ina uwezo kuchunguza uhalifu uliotekelezwa wakati Burundi ilipokuwa mwanachama wa mahakama hiyo.

Lakini haiwezi kuchunguza uhalifu wowote wa siku zijazo.

Hatua hiyo inaweza kuwa mfano na kuonyesha viongozi wengine kwamba kujiondoa katika mahakama hiyo ni njia mojawapo ya kuepuka jicho la kimataifa hadi pale Jamii ya kimataifa itakapochukua hatua na taasisi kama vile Umoja wa Afrika ama baraza la usalama la umoja wa mataifa litakapowafuatilia washukiwa na kuyakumbusha mataifa kwamba kujiondoa katika ICC hakumaanishi moja kwa moja kwamba waathiriwa hawatopata haki.