Msichana wa shule aliyelazimishwa kupaka nywele rangi ashtaki

Schoolgirls in Tokyo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Msichana wa shule aliyelazimishwa kupaka nywele rangi ashtaki

Msichana wa shule mwenye umri wa maiaka 18 nchini Japan anaishtaki manispaa ya mji baada ya shule yake kumlazimisha mara kwa mara kuipaka nyele yake rangi nyeusi nywele ambayo kwa kawaida ni ya rangi ya udhurungi.

Msichana huyo anasema aliambiwa kuwa atalazimika kuihama shule hiyo iliyo karibu na mji wa Osaka iwapo hangefuata agizo lililotaka nywele za wanafunzi kuwa nyeusi.

Inaripotiwa kuwa alisena rangi aliyokuwa akipaka iliharibu nywe yake.

Shule ya upili ya Kaifukan ilisema kuwa sera zake ni za kuwazui wanafunzi kupaka nyele zao rangi tofauti.

Agizo la shule kwa mwanafunzi lilitolewa liocha ya mama yake kuiambia shule kuwa msichana huyo alizaliwa akiwa na nyele ya rangi ya udhurungi.

Ripoti zinasema kuwa msichana huyo hajahudhuria masomo tangu mwezi Septemba mwaka uliopita.

Mwalimu mkuu wa shule ya Kaifukan Masahiko Takahashi hajazungumzia kesi hiyo.

Mada zinazohusiana