Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 29.10.2017

Farhad Moshiri Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Farhad Moshiri

Mfanyabiashara mwenye hisa nyingi zaidi katika klabu ya Everton Farhad Moshiri, anataka kumsaini mchezaji wa Chile Sanchez kwa pauni milioni 30. (Sun on Sunday)

Everton wana mpango wa kumsajili aliyekuwa meneja wa England na Crystal Palace Sam Allardyce. (Sun on Sunday)

Barcelona wana matumani ya kumsaini mchezaji wa safu ya kati raia wa Brazil Philippe Coutinho, kwa pauni milioni 132 mwezi Januari (Sunday Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Philippe Coutinho

Manchester City wana mpango wa kumfanya mchezaji kiungo cha kati raia wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 26, kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi katika historia yake wa Pauni 250,000 kwa wiki (Daily Star Sunday)

Crystal Palace wana mpango wa kumsaini mshambuliaji wa Besiktas, Cenk Tosun 26, ambaye thamani yake inaweza kuwa karibu paunia milioni 20 (Mail on Sunday)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David de Gea

Kipa wa Manchester United na Uhispania David de Gea, 26, bado anasuburi kuambiwa na klabu yake kuhusu mazungumzo ya mkataba (Daily Star Sunday)

Meneja wa Manchester United ana hofu kuhusu hali ya mkataba wa Marouane Fellaini. Mkataba wa raia huyo wa Ubelgiji 29, unafikia mwisho, mwishoni mwa msimu. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Jose Mourinho

Mourinnho anapania kumsaini mchezaji raia wa Ubelgiji anayeichezea Paris St-Germain Thomas Meunier 26. (Sunday Express)

Everton wana naia ya kumsaini kijana wa Sheffield United Sam Graham. (Liverpool Echo)