Rapa aonyesha sehemu nyeti 'kimakosa' katika Instagram Live

Rapa wa Afrika Kusini Emtee alikuwa akizungumza na mashabiki wake akiwa katika haja ndogo

Chanzo cha picha, Instagram

Maelezo ya picha,

Rapa wa Afrika Kusini Emtee alikuwa akizungumza na mashabiki wake akiwa katika haja ndogo

Kumekuwa na hisia katika vyombo vya habari vya Afrika Kusini baada ya mwanamuziki mmoja wa taifa hilo Emtee kwa bahati mbaya kuonyesha uume wake katika mtandao wa Instagram Live.

Chombo cha habari cha Times Lives kinasema kuwa rapa huyo ambaye jina lake kamili ni Mthembeni Ndevu hakukubali kudhalilika na kitendo hicho baada ya picha hizo zilizoonyesha sehemu yake nyeti kusambazwa.

Huku mtandao wa burudani wa Zalebs ukisema kuwa watu wamekuwa wakichochea hali hiyo kwa kutumia alama ya reli #emteechallenge.

Mtandao huo unasema kuwa hatua hiyo ni nzuri kwa msani huyo.

''Unajua kwamba umefanya makosa na kupewa changomoto'', unaelezea.

Emtee aliambia Times Lives:Nilikuwa chooni nikijibu maswali ya mashabiki moja kwa moja.Nilitaka kujisaidia haja ndogo lakini bila kufikiria nikatumia mkono huohuo niliokuwa nikishikilia simu yangu wakati nilipokuwa nikiendelea na haja ndogo na kutumia mkono huohuo kupiga picha.Sikufikiria kuhusu kilichofanyika hadi nilipogundua kwamba kile nilichofanya na nikaomba msamaha.