Waandishi wa habari washambuliwa makao makuu ya Upinzani Kenya

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
Image caption Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga

Upinzani nchini Kenya Nasa umeomba msamaha baada ya vijana wanaodaiwa kuwa wa wafuasi wa muungano huo kuwashambulia waandishi wawili wa habari katika makao yake makuu mjini Nairobi.

Katika taarifa, Nasa imesema kuwa itawachukulia hatua waliohusika ikakitaka chombo cha habari kutoa kanda ya video kuhusu kisa hicho ili uchunguzi ufanyike.

Mwandishi wa runinga ya Citizen TV's Francis Gachuri na mpiga picha wa NTV Jane Gatwiri walishambuliwa baada ya vijana hao kudai kutoridhishwa na vituo vyao vilivyorusha matangazo ya marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26.

Kiongozi wa muungano huo Raila Odinga alisusia uchaguzi huo akisema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki na ulikuwa unakiuka sheria za uchaguzi.

Mada zinazohusiana