Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 01.11.2017

Thomas Lemar

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Thomas Lemar

Itawalazimu Arsenal kushindana na Barcelona na pia Liverpool ikiwa wanataka kumsaini wing'a wa Monaco Thomas Lemar ,21 msimu ujao. (Daily Telegraph)

Sam Allardyce atafanya mazungumzo na Everton kuhusu nafasi iliyo wazi ya umeneja lakini anataka mkataba mzuri iki kuchukua nafasi hiyo. (Sun)

Arsenal na Chelsea wote wanammzea mate aliyekuwa kipa wa Liverpool Peter Gulacsi, 27, kutoka RB Leipzig. (ESPN)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Michael Carrivk

Mchezaji wa safu ya kati wa Manchester United Michael Carrivk 36, hana mpango wa kuondoka Old Trafird licha ya Leicester City, West Bromwich Albion na Aston Villa kuonyesha dalili za kutaka kumsaini. (ESPN)

Mshambuliajia wa Swansea Tammy Abraham, 20 ambaye yuko Swansea kwa mkopo atakaa fursa ya kuichezea Nigeria na badala yake kuamua kusubiri kuichezea England. (Times - subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Radja Nainggolan

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Roma Radja Nainggolan anasema kuwa hakufikiria kujiunga na Chelsea, ambao waihusishwa na kumsaini mchezaji huyo wa miaka 29. (Independent)

Mchezaji wa safu ya kati wa Monaco, Fabinho, 24, amefichua kuvunjika kwake moyo baada ya jitihada zake za kuhamia Manchester United na Paris St-Germain kugonga mwamba mwaka uliopita. (Sports Illustrated)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Claudio Ranieri

Leicester City hawakuwasiliana na meneja wa zamani Claudio Ranieri, ambaye sasa anaongoza klabu ya Ufaransa Nates, kuhusu kurejea kwake katika klabu hiyo kama meneja. (Leicester Mercury)

Manchestrer United ndio wanaweza kumsaini mlinzi wa Celtic Kieran Tierney, 20, na mshambuliaji wa umri wa miaka 21 Moussa Dembele. (Mirror)