Wafugaji wa Kenya wapata hasara kwa kuingiza ng'ombe wao Tanzania

Kutokana na ukame unaendelea katika baadhi ya maeneo nchini Kenya imelazimisha baadhi ya wafugaji kuvusha mifugo yao kuingia nchi jirani ya Tanzania .

Serikali ya Tanzania inasema hatua hiyo ni kinyume cha sheria kwa madai kwamba wafugaji hao wanapaswa kupata kibali kwanza cha kuingiza mifugo yao kwenye nchi jirani.

Tayari serikali ya Tanzania imeanza operesheni ya kuwarudisha wafugaji wasio na kibali na mifugo yao kule walikotoka kama anavyoarifu mwandishi wetu Imanuel Igunza.