Orodha ya wanaowania taji la mchezaji bora Afrika yatolewa bila mshindi wa 2016 Riyad Mahrez

Riyad Mahrez alishinda mchezaji bora 2016
Image caption Riyad Mahrez alishinda mchezaji bora 2016

Shirikisho la soka barani Afrika limetoa orodha ya wachezaji 30 watakaowania taji la mchezaji bora wa soka barani Afrika mwaka huu.

Mshambuliaji wa Gabon Pierre Erick Aubameyang aliyeshinda mwaka 2015 ameorodheshwa pamoja na nyota kadhaa wanaosakata dimba barani Ulaya kama vile mshambuliaji wa Senegal na Liverpool Sadio Mane ambaye alikuwa katika nafasi ya tatu 2016.

Mshindi wa mwaka 2016 Riyad Mahrez wa Algeria hakuorodheshwa katika orodha hiyo.

Kati ya wachezaji 30 waliorodheshwa ni saba pekee ambao hawachezi soka yao barani Ulaya, huku kipa wa Misri aliye na umri wa miaka 44 pia akiorodheshwa.

Kipa huyo wa miaka mingi anacheza soka yake katika klabu ya Al-Taawoun nchini Saudi Arabia.

Kwengineko Mahrez ameshindwa kuonyesha umahiri wake ambao alionyesha wakati alipokuwa kiungo muhimu wa klabu ya Leicester na kuiwezesha kushinda ligi ya Uingereza

Huwezi kusikiliza tena
Riyad Mahrez ashinda tuzo ya BBC ya mchezaji bora Afrika

Wachezaji wanne wanaosakata soka yao Afrika wameorodheshwa kuwania taji la mchezaji bora wa bara Afrika mbali na mchezaji bora anayesakata soka barani humu.

Wachezaji hao ni mchezaji wa Tunisia Ali Maaloul (Al Ahly), mchezaji wa Afrika Kusini Percy Tau, Kipa wa Uganda Dennis Onyango (wote wa Mamelodi Sundowns) na Fackson Kapumbu wa Zambia anayeichezea klabu ya (Zesco United).

Washindi wa mataji hayo watatangazwa katika mji mkuu wa Ghana Accra mnamo tarehe 4 mwezi January 2018.

Kura zitakazopigwa na makocha, wakurugenzi wa kiufundi kutoka mataafa mbali mbali pamoja na wanachama wa kiufundi wa Caf na kamati endelvbu mbali na jopo la waandishi zitabaini washindi.

  • Orodha ya wachezaji wa taji la mchezaji bora Afrika

Vincent Aboubakar (Cameroon & Porto), Karim El Ahmadi (Morocco na Feyenoord), Christian Atsu (Ghana & Newcastle), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Borussia Dortmund), Eric Bailly (Cote d'Ivoire na Manchester United), Cedric Bakambu (DR Congo na Villareal), Keita Balde (Senegal & Monaco), Christian Bassogog (Cameroon na Henan Jianye), Yves Bissouma (Mali na Lille), Khalid Boutaib (Morocco na Yeni Malatyaspor), Yacine Brahimi (Algeria na Porto), Essam El Hadary (Egypt na Al Taawoun), Junior Kabananga (DR Congo na Astana), Fackson Kapumbu (Zambia na Zesco), Naby Keita (Guinea na RB Leipzig), Ali Maaloul (Tunisia na Al Ahly), Sadio Mane (Senegal na Liverpool), Moussa Marega (Mali na Porto), Victor Moses (Nigeria na Chelsea), Youssef Msakni (Tunisia na Al Duhail), Michael Olunga (Kenya na Girona), Fabrice Ondoa (Cameroon na Sevilla), Denis Onyango (Uganda na Mamelodi Sundowns), Thomas Partey (Ghana na Atletico Madrid), Mohamed Salah (Egypt na Liverpool), Mbwana Samata (Tanzania na Genk), Jean Michel Seri (Cote d'Ivoire na Nice), Percy Tau (South Africa na Mamelodi Sundowns), Bertrand Traore (Burkina Faso na Lyon), William Troost-Ekong (Nigeria na Bursaspor)

  • Mchezaji bora wa Afrika anayesakata soka barani humu

Nasr Eldin Ahmed (Sudan & Hilal Obeid), Junior Ajayi (Nigeria & Al Ahly), Karim Aouadhi (Tunisia & CS Sfaxien), Aristide Bance (Burkina Faso & Al Masry), Alkhaly Bangoura (Guinea & Etoile du Sahel), Achraf Bencharki (Morocco & Wydad Athletic Club), Jeremy Brockie (New Zealand & Supersport), Fawzi Chaouchi (Algeria & MC Alger), Oussama Darfalou (Algeria & USM Alger), Muaid Ellafi (Libya & Ahly Tripoli), Tady Etekiama (DR Congo & AS Vita), Ahmed Fathi (Egypt & Al Ahly), Dean Furman (South Africa & Supersport United), Sylvain Gbohouo (Cote d'Ivoire & TP Mazembe), Tarek Hamed (Egypt & Zamalek), Fackson Kapumbu (Zambia & Zesco), Saber Khalifa (Tunisia & Club Africain), Taha Yassine Khenissi (Tunisia & Esperance), Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly), Ayman Majid (Morocco & FUS Rabat), Ben Malango (DR Congo & TP Mazembe), Aymen Mathlouthi (Tunisia & Etoile du Sahel), Mohamed Meftah (Algeria & USM Alger), Sabelo Ndzinisa (Swaziland & Mbabane Swallows), Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns), Mohamed Ounnajem (Morocco & Wydad Athletic Club), Elsamani Saadeldin (Sudan & Al Merreikh), Saladin Said (Ethiopia & Saint George), Geoffrey Serunkuma (Uganda & KCCA), Percy Tau (South Africa & Mamelodi Sundowns).

Mada zinazohusiana