Aliyetekeleza shambulizi la New York afikishwa mahakamani

Sayfullo Saipov katika picha ya mwaka 2016
Maelezo ya picha,

Sayfullo Saipov katika picha ya mwaka 2016

Waendesha mashtaka mjini New York wamefungua mashtaka dhidi ya mhamiaji kutoka nchini Uzbek anayedaiwa kuhusika katika shambulio la gari dogo la mizigo lilitokea jana na kuua watu nane katika mji wa New York nchini Marekani.

Sayfullo Saipov anakabiliwa na mashtaka ya kuwasambazia vifaa kundi la kigaidi la Islamic State.

Maelezo ya picha,

Eneo ambalo shambulizi lilifanyika

Waendesha mashtaka mjini New York wamefungua mashtaka dhidi ya mhamaji kutoka nchini Uzbestan anayedaiwa kuhusika katika shambulio la gari dogo la mizigo lilitokea jana na kuua watu nane katika mji wa New York nchini Marekani.

Sayfullo Saipov anakabiliwa na mashtaka ya kusaidia kutoa vifaa kwa kundi la kigaidi la Islamic State.

Akizungumzia mashataka yaliyofunguliwa kaimu mwanasheria mkuu JOON Kim amesema Saipov amefunguliwa mashitaka ya makosa mawili ya ugaidi.

Maelezo ya picha,

Wanausalama wakisaidia majeruhi katika eneo hilo

Shitaka la kwanza ni kutoa vifa vya kusaidia maandalizi ya shambulio la kigaidi kwa kundi la IS, na shitaka la pili kusababisha uharibifu wa magari ambayo yalisabisha vifo na majeruhi.

Naye Rais Donald Trump akionekana na baraza lake katika ikulu ya white house, amesema kuwa anatarajia kuchukua hatua za haraka dhidi ya mfumo wa uhamiaji nchini humo.

Hata hivyo Rais Trump ametaka adhabu kali kutolewa dhidi ya watu wanaobainika kujihusisha katika vitendo vya kigaidi, kama hili la New York.

Awali Gavana wa New York, Andrew Cuomo, alimlaumu Rais Trump kwa madai kuwa anatumia tukio hilo kwa kujinufaisha kisiasa.