Kim Jong-Un atembelea kiwanda cha vipodozi na mkewe

Kim Jong-Un atembelea kiwanda cha vipodozi na mkewe Haki miliki ya picha KCNA VIA REUTERS
Image caption Kim Jong-Un atembelea kiwanda cha vipodozi na mkewe

Kiongozi wa Korea kazkazini Kim Jong un ametembelea kiwanda kimoja cha vipodozi mjini Pyongyang akiandamana na mkewe Ri Sol-ju na dadake Kim Yoo-jong.

Vyombo vya habari vya taifa hilo vimeonyesha picha zisizo na tarehe kuhusu ziara hiyo siku ya Jumapili.

Wanawake wote wawili huwa ni nadra kuonekana hadharani.

Kuonekana hadharani kwa bi Kim kunajiri muda mfupi baada ya kuongezwa madaraka katika serikali ya Korea kaskzini.

Bidhaa za kigeni za kifahari ikiwemo vipodozi vimeadimika nchini Korea Kaskazini kufuatia vikwazo kadhaa vya Umoja wa Mataifa.

Ni Kwa nini alitembelea kiwanda hicho cha vipodozi?

Kwa miaka mingi mataifa mengi yamesita kuuza bidhaa za anasa nchini Korea Kaskazini kutokana na vikwazo.

Hatua hiyo imeilazimu Korea Kaskazini kuanzisha viwanda vya kutengeza vipodozi vyake huku bidha kama vile Bomhyanggi na Unhasu zikipata umaarufu kutoka kwa wateja.

Ijapokuwa anajulikana sana kwa picha zake katika maeneo ya kijeshi mbali na yale ya kufanyia majaribio makombora, ziara ya bwana Kim katika kiwanda cha kutengeza vipodozi inatoa ujumbe wa propaganda katika kuhalalisha uongozi wake miongoni mwa watu matajiri na wale uwezo wa kadri.

Haki miliki ya picha KCNA VIA AFP
Image caption Kiongozi wa Korea kazkazini Kim Jong un ametembelea kiwanda kimoja cha vipodozi mjini Pyongyang akiandamana na mkewe Ri Sol-ju na dadake Kim Yoo-jong

Amepigwa picha mara kwa mara katika viwanda pamoja na maneo muhimu ya uchumi wa Korea Kaskazini , huku vyombo vya habari vya serikali vikisema kuwa taifa hilo limepiga hatua katika uzalishaji wa runinga za 3D na simu aina ya smartphone.

Ziara hiyo ni ya kuonyesha kwamba Korea Kaskazini inaweza kutegemea raia wake na kuendelea katika viwango vinanvyoonyeshwa na Beinjing na Seoul, mchambuzi wa Korea Kaskazini Ankit panda aliambia BBC.

Hata iwapo tunajua sio kweli , ni muhimu kwa taifa hilo kuwaonyesha watu wake kwamba inaweza kutengeza bidhaa za kujifurahisha.

Wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho cha vipodozi kilichopo Pyongyang, bwana Kim alikisifu kiwanda hicho kwa kuzalisha vipodozi vya hali ya juu mbali na kuimarisha hali yake na kufikia viwango vya kimataifa, kulingana na chombo cha habari cha KCNA.

Kwa nini Kim Jong Un alizuri kiwanda hicho akiandamana na mkewe na dadake?

Akiwa amevalia rinda lenye rangi nyeupe na nyeusi, bi Ri ameonekana sana katika picha hizo.

Lakini mkewe Kim haonekana katika picha hiyo licha ya ripoti za vyombo vya habari za KNCA kusema kuwa alikuwepo pamoja na maafisa wengine wakuu.

Ni machache yanayojulikana kuhusu familia ya bwana Kim na maisha yake ya kibinafsi, na watu wa familia yake hawaonekani hadharani.

Kuonekana hadharani kwa bwana Kim huwa kunafanywa kwa mpangilio.

Haki miliki ya picha KCNA VIA REUTERS
Image caption Lakini mkewe Kim haonekana katika picha hiyo licha ya ripoti za vyombo vya habari za KNCA kusema kuwa alikuwepo pamoja na maafisa wengine wakuu.

Bwana Panda aliambia BBC kwamba ni muhimu kwamba aliamua kuonekana hadharani na mkewe pamoja na dadake wakati huu.

''Kunasisitiza umuhimu wa familia yake pamoja na familia na kwamba uhusiano wa damu ni muhimu sana kwake, na kwamba wanawawe ndio watakaomrithi'', alisema Panda.

Kufuatia hatua yake ya kupandishwa cheo, uwepo wa Bi Kim katika ziara hiyo unamaanisha kwamba utawala wa Kim unataka ulimwengu kuona kwamba pia yeye yupo katika wadhfa wa juu .

Mapema mwezi huu Bwana Kim alimweka dadaake katika bodi yenye maamuzi makuu , kwa jina Politburo.

Haki miliki ya picha KCNA VIA REUTERS
Image caption Rais Kim Jong un katika kiwanda cha vipozi mjini Pyongyang

Ziara hiyo ilifanyika wakati ambapo kulikuwa na hali ya wasiwasi katika rasi ya Korea kuhusu misururu ya majaribio ya makombora na silaha za nyuklia mbali na vita vya maneno kati ya Kim Jong un na rais wa Marekani Donald Trump ambaye anatarajiwa kufanya ziara nchini Korea Kusini katika kipindi cha wiki moja ijayo

Ziara hiyo ya rais wa Korea Kaskazini ilitangazwa katika vyombo vya habari vya taifa hilo, siku moja baada ya waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis kusema kuwa Marekani haitakubali Korea Kaskazini iliojihami na silaha za kinyuklia.

Bwana Mattis ambaye alikuwa ziarani barani Asia na ambaye alitarajiwa kuzuru mjini Seoul siku ya Jumamosi alisisitiza msimamo wa Marekani kwamba utumizi wowote wa silaha za kinyuklia wa Korea Kaskazini utajibiwa na nguvu kali za kijeshi.

Mada zinazohusiana