Mourinho afika mahakamani kujibu madai ya kukwepa kulipa kodi Uhispania

Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho

Mkufunzi wa Man United Jose Mourinho amewasili katika mahakama ya Uhispania kujibu madai ya kukwepa kulipa kodi wakati alipokuwa mkufunzi wa klabu ya Real Madrid.

Wawakilishi wake wamekana kuwa anadaiwa Yuro milioni 3.3 kupitia haki za matangazo ambazo hakuzitangaza.

Bwana Mourinho alionekana akiingia mahakamani katika makaazi ya mjini Madrid Pozuelo de Alarcon.

Kusikizwa kwa kesi hiyo kunajiri siku mbili kabla ya Manchester United kucheza dhidi dhidi ya Chelsea katika ligi ya Uingereza.

Mkufunzi huyo alizungumza na vyombo vya habari siku ya Alhamisi kama ilivyo ada.

Utawala wa Uhispania ulianzisha kesi dhidi ya Mourinho mnamo mwezi Juni.