Simba ''wapenzi wa jinsia moja'' wapigwa picha Kenya

Simba wapenzi wa jinsia moja wapigwa picha katika mbunga ya wanyama pori ya Masai Mara Kenya
Maelezo ya picha,

Simba wapenzi wa jinsia moja wapigwa picha katika mbunga ya wanyama pori ya Masai Mara Kenya

Picha moja ya simba wawili wa kiume walioonekana katika mbuga moja ya wanyama nchini Kenya wakifanya tendo la ngono imezuia hisia kali nchini humo.

Tayari afisa wa bodi simamizi ya udhibiti wa filamu Kenya anasema kuwa wanyama hao huenda wamejifunza tabia hiyo kutoka kwa binadamu.

''Wanyama hawa wanahitaji kupitia ushauri nasaha kwa sababu huenda wamejifunza tabia hii kwa wapenzi wa jinsia moja wanaozuru mbuga hizo na kufanya tabia mbaya''', aliseama Ezekiel Mutua , ambaye ni afisa mkuu mtendaji wa bodi ya kukagua viwango vya filamu nchini Kenya KFCB.

Matamshi ya Mutua yanajri baada ya picha zilizopigwa na mpiga picha wa Uingereza Paul Goldstein kuonyesha simba wawili wa kiume wakielekea katika kichaka katika mbuga ya Masai Mara iliopo kusini magharibi mwa Kenya .

Maelezo ya picha,

Ujumbe wa Ezekiel Mutua katika mtandao wa twitter

Simba mmoja alionekana akilala chini na mwengine kumpandia juu.

Wakati simba wanapofanye tendo la ngono huwachukua sekunde chache pekee, lakini wawili hao walifanya tendo hilo kwa takriban dakika moja huku hisia za mapenzi zilizoonekana baada ya tendo hilo zikithibitisha wanayvyopendana, ikifananishwa na vurugu baada ya simba mke na dume kujamiana'', alisema mpiga picha huyo.

Mutua hujulikana kama mwanaharakati wa kupigania maadili nchini Kenya na tayari amewahi kupiga marufuku vipindi vya runinga vinavyodaiwa kukuza mapenzi ya jinsia moja.

Afisa huyo ametaka utafiti wa kisayansi kufanyiwa simba hao kubaini chanzo cha wawili hao kushiriki katika tendo kama hilo.

Maelezo ya picha,

Watoto wa simba katika mbuga ya Masai Mara Kenya

Anasema kuwa tabia hiyo huenda inatokana na kutawaliwa na mashetani.

''Duniani ushawahi kusikia kitendo kama hiki kikitokea.Mapepo ambayo huwatawala binadamu sasa yameanza kuwaingia wanyama'', alisema Mutua.

''Hiyo ndio sababu ninataka wanyama hao kutengwa, na watafiti kuangazia tabia zao iwapo ni za kawaida''.