Kiongozi wa genge auawa Mexico akibadili sura

Jesus Martin au El Kalimba amekuwa akisakwa na polisi kwa kuendesha biashara ya kuiba mafuta kwa kukata mabomba ya usafirishaji wa bidhaa hiyo muhimu.
Maelezo ya picha,

Jesus Martin au El Kalimba amekuwa akisakwa na polisi kwa kuendesha biashara ya kuiba mafuta kwa kukata mabomba ya usafirishaji wa bidhaa hiyo muhimu.

Kiongozi mmoja wa genge nchini Mexico ameuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa katika kliniki akifanyiwa upasuaji wa kubadili sura yake mbali na kuondosha alama zake za vidole.

Maafisa wanasema kwamba watu walio na silaha walivamia kliniki hiyo ya mjini Puebla na kumfyatulia risasi kiongozi huyo wa genge Jesus Martin, anayejulikana pia kwa jina la mtaani El Kalimba.

Maafisa hao wanaendelea kueleza tathmini yao kwamba tukio hilo ni baada ya ugomvi baina ya magenge hasimu ambapo pia watu wengine watatu wamefariki .

Jesus Martin au El Kalimba amekuwa akisakwa na polisi kwa kuendesha biashara ya kuiba mafuta kwa kukata mabomba ya usafirishaji wa bidhaa hiyo muhimu.

Ukubwa wa biashara hiyo umefananishwa na ile ya ulanguzi wa mihadarati nchini Mexico.