Waziri mkuu wa Lebanon ajiuzulu akihofia maisha yake

Waziri mkuu wa Lebanon Saad al-Hariri
Image caption Waziri mkuu wa Lebanon Saad al-Hariri

Waziri mkuu wa Lebanon Saad al-Hariri ametangaza kujiuzulu katika hatua ya kushangaza akisema kuwa anahofia maisha yake.

Katika mkutano na vyombo vya habari katika mji mkuu wa Saudia Riyadh, bwana Hariri alilikosoa kundi la madhehebu ya Shia Hezbollah na Iran akisema kuwa hakuna eneo ambalo Iran itaelekea bila kupanda hofu na uharibifu .

Amesema kuwa hali ya sasa nchini Lebanon ni sawa na ilivyokuwa wakati babake Rafiq alipouawa 2005 na kwamba alikuwa anahisi kuna njama ya kumuangamiza.

Waandishi wanasema kuwa ni muhimu kwamba bwana Hariri hakuwa akizungumza kutoka Beirut bali kutoka Saudia ambayo ni mkosoaji mkubwa wa Iran.

Mada zinazohusiana