Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 05.11.2017

Alexis Sanchez

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Alexis Sanchez

Bayern Munich wamekana kuwa mbioni kumsaka nyota wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, kwa sababu wanaamini kuwa tayari ameamua penye anataka kweda.(Metro)

Kiungo wa kati Cesc Fabregas, 30, amethibitisha kuwa anataka kusaini mkataba mpya na Chelsea licha ya Manchester United kuonyesha nia ya kumsaini.(London Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Harry Kane

Real Madrid wanatathmini ikiwa watawawinda wachezaji wa Tottenham Harry Kane, 24, na Dele Alli, 21, baada ya kuonyesha michezo misafi dhidi ya mabingwa hao wa Uhisapnia. (Marca)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino pia amehusishwa na Real Madrid lakini amesema kuwa yuko katika klabu nzuri zaidi duniani. (Observer)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Antonio Conte

Meneja wa Chelsea Antonio Conte atakuwa lengo la AC Milan ikiwa klabu hiyo ya Italia itaamua kumfuta Vincenzo Montella. (Sunday Express)

Alvaro Morata anasema alikuwa na fursa ya kujiunga na Manchester United msimu huu lakini akaamua kujiunga na Chelsea kwa walimuonyesha kuwa kweli walikuwa wanamhitaji . (The Independent)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka nyongeza ya mshahara wa pauni milioni 3 kwa mwaka kwenye klabu yake ya sasa. (Sunday Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jose Mourinho

Mchezaji wa kiungo cha kati Fernandinho, 32, anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa miezi 12 na Manchester United. (Daily Star)

Arsenal wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa mahasimu Tottenham kumsaini mchezaji wa kiungo cha kati wa Schalke Leon Goretzka ,22, (Sunday Mirror)

Everton wamejiunga na Machester United katika mbio za kumpata mchezaji wa West Brom Jonny Evans, 29. (Sun on Sunday)