Kimbunga Damrey chasababisha vifo vya watu 27 Vietnam

Chanzo cha picha, Reuters
Barabara nyingi hazipitiki au ni hatari kupitia
Kimbunga kwa jina Damrey ambacho kimekuwa kikipiga maeneo ya kusini na kati ya Vietnam kimesababisha vifo vya watu 27, na wengine zaidi ya 20 hawajulikani waliko.
Kimbunga hicho kilifika maeneo ya bara Jumamosi kikiwa na upepo unaovuma kwa kasi ya kilomita 90 kwa saa.
Nyumba zaidi ya 40,000 zimeharibiwa vibaya na maelfu ya watu wamehamishwa makwao.
Maeneo mengi pia hayana umeme.
Eneo lililoathiriwa zaidi ni jiji la Nha Trang - umbali wa 500km hivi kusini mwa jiji la Da Nang katika pwani ya nchi hiyo ambapo viongozi wa mataifa wanachama wa Apec (Jumuiya ya Kiuchumi ya Asia na Pasific) wanatarajiwa kuhudhuria mkutano mkuu baadaye wiki hii.
Chanzo cha picha, Reuters
Watu wakitumia baiskeli kusafiri kupitia barabara za mji wa Hue, Vietnam
Chanzo cha picha, AFP
Mji wa kitalii wa Hoi An pia umeathiriwa sana
Chanzo cha picha, Reuters
Mji wa Nha Trang hali imekuwa hivi
Chanzo cha picha, AFP
Mji ulioanguka na kufunga barabara Nha Trang
Chanzo cha picha, EPA
Wataalamu wa hali ya hewa wanasema kimbunga hicho ni miongoni mwa vimbunga vyenye uharibifu mkubwa kuwahi kukumba eneo hilo katika miongo kadha
Chanzo cha picha, Reuters
Paa la nyumba ambalo limeharibiwa Ho Chi Minh