Mgahawa unaotumia lugha ya ishara Tanzania

Mgahawa unaotumia lugha ya ishara Tanzania

Nyanda za juu kusini mwa Tanzania, mkoani Iringa kuna mghahawa wa kipekee unaofahamika kwa jina Neema Craft.

Katika Mgahawa huu watoa huduma wote ni viziwi, wanatumia lugha ya ishara kuwasiliana na wateja.

Mwandishi wa BBC Esther Namuhisa ameutembelea mgahawa huu ambao umepata umaarufu hasa kwa watalii na wenyeji.