Kipimo cha pumzi kugundua Malaria chaonyesha matumaini

Kipimo cha pumzi kugundua Malaria chatoa matumaini

Chanzo cha picha, WASHINGTON UNIVERSITY

Maelezo ya picha,

Kipimo cha pumzi kugundua Malaria chatoa matumaini

Watu wanaougua ugonjwa wa malaria sasa watalazimika kupimwa kwa kutumia pumzi zao kulingana na wanasayansi wa Marekani.

Tayari walikuwa wametumia mfano wa kifaa cha kutumia pumzi barani Afrika, mkutano wa dawa za kitropiki ulielezewa.

Kifaa hicho kilionekana kuwa imara katika kuwapima watoto lakini kitahitaji kuimarishwa zaidi ili kutumiwa mara kwa mara.

Miongoni mwa harufu inazotoa ni sawa na ile inayowavutia wadudu wanaosambaza ugonjwa wa malaria.

Miti aina ya Pine na ile ya Conifers hutoa harufu hiyo ili kuwavutia mbu pamoja na wadudu wengine kulingana na watafiti kutoka chuo kikuu cha Washington mjini St. Louis .

Wanaamini kwamba watu wanaougua ugonjwa wa malaria ambao hutoa harufu hiyo wakati wanapopumua pia wao huvutia mbu na kuwaambukiza wadudu hao wanapowauma, hatua ambayo hupelekea kusambazwa kwa ugonjwa huo na mbu.

Ijapokuwa kipimo hicho kinahitaji kuimarishwa, kinaweza kutoa mwelekeo mpya na rahisi wa kuugundua ugonjwa huo, profesa Audry Odom John na wenzake wanasema.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kipimo hicho cha kutumia hewa ya mtu anapopumua kinaweza kugundua harufu sita tofauti ili kubaini visa vya malaria.

Kipimo hicho cha kutumia hewa ya mtu anapopumua kinaweza kugundua harufu sita tofauti ili kubaini visa vya malaria.

Watafiti hao walijaribu sampuli kadhaa za vipimo hivyo kutoka kwa watoto 35 wenye homa nchini Malawi wengine wakiwa na malaria wengine wakiwa bila ugonjwa huo.

Kilitoa vipimo sawa miongoni mwa watoto 29, ikimaanisha kiliweza kufanikiwa kwa asilimia 83.

Hatahivyo Matokeo hayo ni ya chini sana kwa kifaa hicho kutumika mara kwa mara , lakini watafiti wana imani kwamba wanaweza kukiimarisha na kuanza kuuzwa madukani.