Watu wenye Silaha wavamia kituo cha Runinga, Afghanistan

Operesheni ya kiusalama inaendelea kwa sasa katika eneo la mashambulio hayo

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Operesheni ya kiusalama inaendelea kwa sasa katika eneo la mashambulio hayo

Watu wenye silaha wamevamia kituo kimoja cha Runinga mjini Kabul Afghanistan na kumuuwa mtu mmoja.

Washambuliaji watatu, waliingia kwa nguvu ndani ya jumba ambalo mna kituo cha Runinga cha Shamshad, baada ya kulipua vilipuzi.

Mlinzi na mmoja wa washambuliaji wanasemekana kuuwawa, huku operesheni ya kiusalama ingali ikiendelea.

Idadi kamili ya majeruhi bado haijajulikana.

Inaaminika kuwa kundi linalojiita Islamic State, ndilo lililohusika na uvamizi huo, hayo ni kwa mjibu wa shirika moja la habari Nchini Afghanistan, Amaq.

Mwaandishi wa BBC katika eneo hilo anasema kuwa hadi sasa anasikia milio ya risasi, kwani mshambuliaji mmoja aliyesalia anaendelea kukabiliana na walinda usalama.

'Nilifaulu kuhepa'

Shamshad TV ilizima mara tu baada ya shambulio hilo kuanza.

"Badhi ya wafanyikazi wenzangu wameuwawa na wengine kujeruhiwa. Nilifaulu kuhepa," Hashmat Istankzai, ripota wan kituo kimoja kinacjhotangaza kwa lugha ya Pashto, ameiambia BBC.

Shamshad TV, ina vipindi vingi vinavyotangazwa kwa lugha nyingi nchini Afghanistan, ikiwemo taarifa ya Habari kwa lugha ya Pashto.

Ni mojawepo ya vituo vinavyoshirikiana na BBC.

Mji mkuu, Kabul umekuwa ukilengwa mara kwa mara hasa katika miezi ya hivi karibuni, mashambulio ambayo yanateklezwa na wanamgambo wa Taliban na wapiganaji wanaojiita Islamic State.

Tishio kwa wanahabari

Afghanistan ni mojawepo ya mataifa hatari zaidi kwa waandishi habari na wafanyikazi wengine wa vyombo vya habari.

Miezi sita ya kwanza ya mwaka huu wa 2017, kulishuhudiwa ghasia kubwa zaidi dhidi ya waandishi habari, huku shirika moja la uchunguzi nchini humo, Afghan Journalists Safety Committee, likirekodi visa 73, ongezeko la asilimia 35% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliotangulia wa 2016.

  • Mwezi Mei mwaka huu, Dereva mmoja wa BBC alikuwa miongoni mwa zaidi ya watu 150 waliouwawa, katika shambulio baya na kubwa zaidi la kujitoa mhanga, lililofanyika katika mji mkuu Kabul.
  • Pia mwezi huo huo wa Mei, IS walilenga Jumba lililo na runinga inayomilikiwa na serikali ya Afghanistan, katika mji wa Jalalabad, na kuwauwa watu 6.
  • Mwaka jana, wafanyikazi 7 wakituo kimoja cha kibinafsi cha runinga, cha Tolo TV waliuwawa na mhanga wa kujitoa kufa wa kundi la Taliban Mjini Kabul.
Maelezo ya picha,

Orodha ya Majina ya Wahabari waliuwawa Afghanistan tangu mwaka 2016