Hofu yawakumba wakaazi India, 'huku ukungu' ukirejea Delhi

Mtumiaji wa Twitter 'MaanviNarcisa' alipiga picha hizi huko Noida - viungani vya mwa mji mkuu Delhi Haki miliki ya picha MAANVINARCISA
Image caption Mtumiaji wa Twitter 'MaanviNarcisa' alipiga picha hizi huko Noida - viungani vya mwa mji mkuu Delhi

Taharuki imewakumba wakaazi wa mji mkuu wa India, Delhi, baada ya wakaazi wa mji huo kuamka na kukuta, ukungu mzito wa rangi ya kijivujivu, ukikumba mji huo mapema siku ya Jumanne.

Hali ya kuona mbali imekuwa ni shida kubwa, kwani kiwango cha uchafuzi wa hewa kimepanda na kuwa mara 30 zaidi, kuliko viwango vilivyowekwa na shirika la Afya duniani-WHO, kwa baadhi ya maeneo mjini humo.

Chama cha madaktari nchini India, (IMA) kimetangaza ''hali ya tahadhari ya kimatibabu" huku kikiomba utawala nchini India "kufanya kila juhudi, ili kukabiliana na hali hiyo".

Watu wamepiga picha za kila aina na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii, kuelezea uukubwa na upana wa tatizo hilo.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Anant Prabhu‏ anasema kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa ni vigumu kuona majengo marefu

Hivi ndivyo ramani inavyoonyesha upana na hatari ya Ukungu huo.

Image caption Ramani ya hatari ya ukungu Delhi

Naye mkaazi mwingine Paroma Mukherjee‏ amepiga picha hii katika mtandao wake wa kijamii.

Image caption Picha ya mkaazi mwingine Paroma Mukherjee‏