Michael Emenalo aondoka Chelsea baada ya miaka 10

Emenalo aliisakatia dimba timu ya taifa ya Nigeria, kombe la Dunia mwaka 1994

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Emenalo aliisakatia dimba timu ya taifa ya Nigeria, kombe la Dunia mwaka 1994

Mwanakandanda maarufu wa zamani wa Nigeria aliyekuwa akisakata dimba nje ya nchi Michael Emenalo, ambaye alikuwa mmoja wa wakufunzi wa klabu ya soka ya ligi kuu nchini Uingereza, Chelsea, amejiuzulu.

Emenalo amekuwa akifanya kazi hiyo kwa miaka 10 iliyopita.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 52, aliyeichezea timu ya soka ya Nigeria katika mchuano wa kombe la Dunia mwaka 1994, aambapo alijiunga na klabu ya Chelsea mwaka 2007 wakati huo ikiwa chini ya mkufunzi Avram Grant, ambapo aliwahi kucheza mechi kati ya Chelsea na timu ya Maccabi ya Tel Aviv, nchini Israeli.

Alifanya kazi katika idara za kuwatafuta wachezaji wapya wenye vipaji vya soka, pamoja na idara ya mafunzo ndani ya klabu ya Chelsea, kabla ya kupandishwa ngazi na kuwa mkufunzi wa kiufundi mnamo mwaka 2011.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Michael Emenalo akiwa na mkufunzi mwenzake wa Chelsea

Wakati wake akiwa Stamford Bridge, Chelsea aliibuka mshindi katika mashindano ya Champions League mwaka 2012, kunyakua mara tatu taji la Premier League, Mara tatu kombe la FA Cups, Kombe la Ligi kuu barani Ulaya na lile la Europa League.

Emenalo amesema: '' Hii imekuwa uamuzi mgumu mno kuufanya, lakini ninachoamini ni kuwa, ni uamuzi bora kwangu, kwa familia yangu pamoja na klabu pia."

Mkuu wa Chelsea Antonio Conte anassema: ''Ninasikitika sana kumuona Michael akiondoka Chelsea na ningependa kumshukuru na pia ningependa kumshukuru kwa msaada wake wote, tangu alipojiunga na klabu hii."