Mkimbiaji wa Kenya Jemima Sumgong, amepigwa marufuku ya miaka 4 kutoshiriki mbio

Mkenya Jemima Sumgong, amepigwa marufuku ya kutoshiriki shindano lolote kwa muda wa miaka minne
Image caption Mkenya Jemima Sumgong, amepigwa marufuku ya kutoshiriki shindano lolote kwa muda wa miaka minne

Bingwa wa Olimpiki wa mbio za masafa marefu upande wa akina dada marathoni, Mkenya Jemima Sumgong, amepigwa marufuku ya kutoshiriki shindano lolote kwa muda wa miaka minne, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli michezoni.

Kwa mujibu wa shirikisho la riadha nchini Kenya-AK, Sumgong ataanza kutumikia adhabu hiyo kuanzia mwezi April mwaka huu wakati aliposimamishwa kwa muda.

Sumgong ni mwanariadha wa pili wa ngazi ya juu mwanamke kupata adhabu kama hiyo, baada ya bingwa wa mbio za New York na Boston Rita Jeptoo kupigwa marufuku pia.

Bi Sumgong ni mwanariadha wa Kwanza wa Kenya kushinda medali ya dhahabu katika mbio za marathoni za Olimpiki.

Mada zinazohusiana