Saudi Arabia yailaumu Iran kwa kombora lililorushwa Riyadh

Map showing Saudi Arabia, Riyadh and Yemen
Maelezo ya picha,

Ramani ikionyesha Saudi Arabia, Riyadh na Yemen

Mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia Prince Mohammed bin Salman ameilaumu Iran kwa uchokozi wa moja kwa moja wa kijeshi kwa kuwapa makombora waasi nchini Yemen.

Hiki kinaweza kutajwa kuwa kitendo cha kivita, vyombo vya habari vilimnukuu Prince Salman akimumbia waziri wa mashauri ya nchi za wa kigeni wa Uingereza Boris Johnson kwenye mawasiliano ya simu.

Siku ya Jumamosi kombora la masafa marefu lilitunguliwa karibu na mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.

Iran imekana kuwahami waasi wa Houthi, ambao wanapigana na muungo unaoongozwa na Saudi Arabia unaoiunga mkono serikali ya Yemen.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Javad Zarif alisema Jumatatu kuwa uchokozi wa Saudi Arabia ulikuwa ni tisho kwa eneo la Mashariki ya kati.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Prince Mohammed bin Salman

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Houthi

Vyombo vya habari vinavyohusiana na waasi wa Houthi viliripoti kuwa waasi walirusha kombora aina ya Burkana H2 la masafa marefu kwenda kwa uwanja wa kimataifa ya ndege wa King Khaled ulio karibu umbalia kilomita 850 kutoka kwa mpaka na Yemene siku ya Jumamosi.

Saudi Arabia iliripoti kuwa mitambo ya kutungua makombora ililikabili kombora hilo likiwa hewani lakini mabaki yake yalianguka kwenye uwanja wa ndege, hakuna maafa yaliyoripitiwa.

Shirika la Human Rights Watch lilisema kurusha makombora dhidi ya uwanja wa ndege ni uhalifu wa vita