Magufuli awafuta maafisa walioshindwa kujibu kuhusu miradi ya barabara

John Magufuli

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

John Magufuli

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili wa manispaa nchini humo mda baada ya wao kukosa kujibu kwa kina maswali aliyowauliza kuhusu bajeti za miradi ya barabara iliyoko maeneo yao

Katika kanda moja ya video Magufuli alimuuliza Bi Mwantum Kitwana Dau, kueleza ni pesa ngapi zilikuwa zimetengwa kwa miradi ya barabra

Kisha Bi Dau alijibu na kusema kuwa hakuwa akifahamu na hakuwa anataka kudanganya.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ilisema kuwa Bi Duya, ambaye ni mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba na Erasto Aron Mfugale watapewa kazi zingine.

Maafisa hao wawili waliofutwa kazi hawakupatikana kutoa maelezo yoyote.

Wakati wa kipindi kimoja cha majibizano Bi Dau, alisema kuwa anaongoza idara nyingi na hawezi kukumbuka mara moja bajeti kamili ya miradi ya barabara.

Kisha Rais Magufuli akajibu, "Huwezi kuongea nami kwa njia kama hiyo."

Rais Magufuli anafahamika kwa kufanya safari za ghafla kwenye ofisi za serikali hasa zile ambazo anaamini kuwa maafisa wake hawafanyi kazi jinsi inavyostahili.