Sanamu ya mwandishi George Orwell yawekwa BBC

George Orwell statue Haki miliki ya picha PA
Image caption Sanamu ya George Orwell imeweka nje ya jumba la BBC New Broadcasting House

Makao makuu ya BBC mjini London yana mkaazi mpya: yeye ni sanamu refu ya shaba. Sanamu ya mwandishi wa vitabu George Orwell sasa imesimama ndani ya jengo la BBC umbali wa dakika chache kutoka eneo ambapo Orwell alifanyia kazi kama mzalishaji wa vipindi vya redio wakati wa vita vya pili vya dunia.

Lakini ni kitu gani mwandishi huyo wa kitabu cha 1984 alikuwa akifanya BBC?

Vita kazini

Orwel alifanya kazi katika BBC kati ya Agosti mwaka 1941 na Novemba mwaka 1943.

Lakini hata hivyo hakufanya kazi katika jengo la Broadcasting House. Akiwa na miaka 38 alifanya kazi kama msaidiz wa vipindi katika ofisi zilizohusika na matangazo ya lugha za kigeni.

Haki miliki ya picha PA
Image caption George Orwell alifanya kazi BBC kwa miaka miwili

Baada ya mwaka mmoja akiwa mzalishaji wa vipindi katika idara ya matangazo ya nchi za nje kaifanya kazi wakati wa vita.

Orwell tayari alikuwa mwandishi wa habari aliyejulikana na pia mwandishi wa vitabu. Lakini hakuwa akijulikana kote duniani, na baadaye akaandika kitabu cha Shamba la Wanyama na cha 1984 mwaka 1945.

Mwandishi wa maisha yake DJ Taylor anaamini kuwa Orwell alikuwa na lengo la kujiunga na BBC. Afya yake tayari ilikuwa mbaya na ilikuwa wazi kuwa hangeitwa vitani. Nafikiri aliiona BBC kama njia nyingine ya kupigana vita akiwa kazini.

Paropaganda bila uongo

Orwell alitumia muda wake mwingi kuandika makala ya kila wiki yaliyolenga sana India ili kusomwa hewania na wafanyakazi kwa idhaa ya India

Makala hayo ilipatikana na kuchapishwa miaka ya themanini. Makala hayo yalikuwa ni kuhusu jinsi vita viliendelea na hayakuwa na uwezo wowote ya kugeuka kuwa fasihi kubwa,

Image caption Muundaji wa sanamu ya Orwell Martin Jennings

Baada ya karibu mwaka mmoja, wale waliosimamia waliamua kuwa kwa sababu Owell alikuwa muungaji mkono mkubwa wa uhuru wa India, ingekuwa vyema ikiwa jina lake lingehusishwa na matangazo. Uwepo wa Orwell hewani ulichangia propaganda kuonekana kama isiyo propaganda.

Aliwaalika watu kama TS Eliot na EM Forster kutangaz kwenda Asia na akaruhusiwa kwenda hewani ye mwenyewe licha ya Januari mwaka 1943 JB Clark wa lugha ya Mandarin kuandika ilani kuwa sauti ya Orwell haikuwa ya kuvutia kabisa.

Image caption George Orwell alihisi kuwa kfanya kazia BBC ilikuwa ni kama kuwa vitani

Orwel alifarikia mwaka 1950 akiwa na umri wa miaka 46.

Eneo ambapo sanamu ya Orwell ipo limekuwa eneo lisilo rasmi la wavutaji sigara tangu jengo la BBC la Broadcasting House lipanuliwe mwaka 2013

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kitabu cha George Orwell cha 1984 na cha Shamba la Wanyama vilifanya kuwa maarufu duniani

Mada zinazohusiana

Kuhusu BBC