Kituo kinachowapa tabasamu wanaougua fistula Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Kituo kinachowapa tabasamu wanaougua fistula Tanzania

Wanawake wengi wanaokabiliwa na tatizo la Fistula nchini Tanzania wamekuwa wakikata tamaa ya maisha hata wengine kudiriki kutaka kujiua kutokana na unyanyapaa uliomo miongoni mwa jamii.

Katika kurudisha furaha ya wanawake hawa, ambao asilimia kubwa ni mabinti wenye umri mdogo ambao walipata matatizo katika uzazi wa kwanza, Hospital ya CCBRT nchini humo imekuwa ikiwapa ushauri nasaha, elimu na mafunzo ya ufundi, hususani kupitia mradi wake wa Mabinti Centre, ili waweze kujitegemea kiuchumi mara wamalizapo tiba na kuanza maisha mapya.

Halima Nyanza aliwatembelea wakiwa darasani.

Mada zinazohusiana