Uwanja mkuu wa ndege Zimbabwe wapewa jina la Rais Robert Mugabe

Rais Robert Mugabe Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Robert Mugabe

Uwanja mkuu wa ndege nchini Zimbabwe umebadilishwa jina na kupewa rasmi jina la Rais Robert Mugabe.

Uwanja wa Kimataifa wa Harare sasa utaitwa uwanja wa Kimataifa wa Robert Mugabe.

Mtandao mmoja wa habari ulichapisha picha za sherehe hizo zilizofanyika mji mkuu Harare.

Barua kutoka kwa mamlaka za safari za ndege nchini humo kushauri kuhusu mabadiliko hayo ilisambatwa pakubwa kwenye mtandao wa Twitter mwezi Septemba

Mugabe, 93, ameitawala nchi hiyo tangu mwaka 1980.