Tani 12 za cocaine zakamatwa Colombia

President Juan Manuel Santos (2R) in the middle of packages containing cocaine, in Apartado, in the Department of Antioquia, Colombia, 08 November 2017. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Juan Manuel Santos (katikati) alisema kuwa hicho kiwango kikubwa zaidi kuwai kupatikana katika oparesheni moja ya polisi.

Polisi nchini Colombia wamekamata tani 12 za cocaine katika kisa ya kukamatwa kwa kiwango kikubwa zaidi cha madawa ya kulevya katika historia ya Colombia.

Madawa hayo yalipatikana yamezikwa kwenye shmba moja la ndizi kaskazini mwa nchi, karibu na njia zinazotumiwa kusafirisha cocaine kwenda Marekani.

Rais Juan Manuel Santos alisema kuwa hicho kiwango kikubwa zaidi kuwai kupatikana katika oparesheni moja ya polisi.

Oparesheni hiyo ilikuwa ni sehemu ya kulikabili genge lenye nguvu la Gulf Clan, ambalo linahusika na ulanguzi wa madawa ya kulevya.

Polisi walisema kuwa madawa hayo yalikuwa ni ya Dairo Úsuga, anayejulikana pia kama Otoniel, kiongozi wa genge la Gulf Clan, moja ya magenge hatari zaidi nchini Colombia.

Vikosi vya usalama vimejaribu kumkamta Otoniel kwa miaka kadhaa.

Polisi walisema kuwa pia waliwakamata watu wanne na kukadiria kuwa madawa hayo yalikuwa ni ya thamani ya dola milioni 360.

Katika kipindi cha miezi mwili iliyopita, vikosi vya usalama vimemakama tani 20 za cocaine huko Antioquia.

Genge la Gulf Clan liliibuka kutoka kwa makundi ya mrengo wa kulia ambayo yalitawanyika mwaka 2006 kufuatia msamaha wa serikali.

Serikali inasema kuwa zaidi ya wanachama 1,500 wamekamatwa mwaka huu na kamanda wake wa cheo cha pili kuuwawa

Mada zinazohusiana