Lupita Nyong'o alikosoa jarida kwa kuhariri picha yake

Picha iliowekwa katika jarida hilo la mwezi Novemba pamoja na picha alizopiga ambazo zinaonekana akiwa na nywele ndefu.

Chanzo cha picha, Twitter

Maelezo ya picha,

Picha iliowekwa katika jarida hilo la mwezi Novemba pamoja na picha alizopiga ambazo zinaonekana akiwa na nywele ndefu.

Mshindi wa tuzo ya Oscar kutoka Kenya Lupita Nyongo ametuma ujumbe wake katika mtandao wa Twitter akilalamika kufuatia hatua ya Jarida la Uingereza la Grazia kuhariri picha yake na kuufanya uso wake kuwa nyororo ili kuifanya kuafikia vigezo vya masharti ya urembo ya Ulaya.

Aliisambaza picha iliowekwa katika jarida hilo la mwezi Novemba pamoja na picha alizopiga ambazo zinaonekana akiwa na nywele ndefu.

Nyongo pia alitumia alama ya reli ya #dtm{akimaanisha usiguse nywele zangu} ambacho ni kichwa cha wimbo wa Solange kuhusu watu kuheshimu nywele nyeusi.

Msanii huyo pia alihusika katika mzozo mwengine na jarida jingine la Uingereza , la Evening Standard lilipohariri picha yake katika ukurasa wake wa kwanza.

Jarida hilo baadaye liliomba msamaha.