Picha bora kutoka Afrika: 3-9 Novemba 2017

Mkusanyiko wa picha za kuvutia zaidi kutoka Afrika na kuwahusu Waafrika pande mbalimbali duniani.

Rais Uhuru Kenyatta (L), Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby (C), na kiongozi wa mrengo wa upinzani National Super Alliance (NASA) Raila Odinga (R) wasimama kupigwa picha baada ya sherehe katika kanisa la All Saints Anglican Church Nairobi, Kenya Novemba 5, 2017. Haki miliki ya picha Reuters

Jumapili, Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby alikuwepo katika kanisa la Kiangilikana la All Saints, Nairobi. Alikutana na Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA) Raila Odinga.

Wakaazi wa Ivory washirikikatika tamasha la Abissa mjini Grand-Bassam, Ivory Coast, 04 Novemba 2017. Sherehe ya Abissa, sherehe ya furaha iliyopangwa na jamii ya N'Zima kuashiria dhana ya demokrasia na haki ya kijamii. Sherehe hii huathimishwa na Jamii ya N'Zima, wenye asili ya Ghana, kila mwisho wa mwezi wa Oktoba na mwanzo wa mwezi wa Novemba, kama ishara ya kuomba msamaha kwa udhalimu uliotendewa jamii hii. Haki miliki ya picha EPA

Tamasha ya kutubu na kufurahia iliadhimishwa nchini Ivory Coast siku ya Jumamosi...

Wakaazi wa Ivory Coast washiriki katika tamasha la Abissa mjini Grand-Bassam, Ivory Coast, 04 Novemba 2017. Sherehe ya Abissa, ni sherehe ya kutubu na kufurahia iliyopangwa na jamii ya N'Zima wenye asili ya Ghana, kuashiria dhana ya demokrasia na haki ya kijamii. Sherehe hii huathimishwa kila mwisho wa mwezi wa Oktoba na mwanzo wa mwezi wa Novemba, kama ishara ya kuomba msamaha kwa udhalimu uliotendewa jamii hii. Haki miliki ya picha EPA

Jamii ya N'zima wanashiriki tamasha hii iitwayo Abissa au tamasha ya kuuliza swali. Inaitwa hivi kwa sababu wao hujiuliza: Je, jamii ya N'zima inastahili kuuona mwaka mpya?...

Awoulae TANOE Amon mfalme wa Grand-Bassam anasafirishwa wakati wa tamasha la Abissa nchini Ivory Coast, 04 Novemba 2017. Wakaazi wa Ivory Coast washiriki katika tamasha la Abissa mjini Grand-Bassam, Ivory Coast, 04 Novemba 2017. Sherehe ya Abissa, ni sherehe ya kutubu na kufurahia iliyopangwa na jamii ya N'Zima wenye asili ya Ghana, kuashiria dhana ya demokrasia na haki ya kijamii. Sherehe hii huathimishwa kila mwisho wa mwezi wa Oktoba na mwanzo wa mwezi wa Novemba, kama ishara ya kuomba msamaha kwa udhalimu uliotendewa jamii hii. Haki miliki ya picha EPA

Mfalme na mwanawe wanabebwa mjini Grand Bassam...

Wakaazi wa Ivory Coast washiriki katika tamasha la Abissa mjini Grand-Bassam, Ivory Coast, 04 Novemba 2017. Sherehe ya Abissa, ni sherehe ya kutubu na kufurahia iliyopangwa na jamii ya N'Zima wenye asili ya Ghana, kuashiria dhana ya demokrasia na haki ya kijamii. Sherehe hii huathimishwa kila mwisho wa mwezi wa Oktoba na mwanzo wa mwezi wa Novemba, kama ishara ya kuomba msamaha kwa udhalimu uliotendewa jamii hii. Haki miliki ya picha EPA

Wakiwa wamevalia mavazi ya waliowadhulumu mwaka uliopita, wanacheza kwa sauti za chombo cha mziki aina ya tam-tam. Punde makosa yote yamesamehewa, wanafurahia mwaka mpya.

Mwanamziki kutoka Nigeria Lamoj, almaarufu kama pepo la Fela, anaimba wakati wa maonyesho ya biashara mjini Lagos Novemba 4, 2017. Lamoj anajiandaa kutoa kanda ya mziki inayoiga mtindo wa mwanamziki maarufu wa afrobeat aliyeaga dunia Fela Anikulakpo-Kuti. Haki miliki ya picha AFP

Siku iyo hiyo, Lamoj ambaye ni mwanamziki wa muziki wa Afrobeat alicheza katika maonyesho ya kibiashara jijini Lagos, Nigeria.

Wakristo nchini Zimbabwe wanacheza ngoma wakisubiri hotuba ya bibi wa rais, Grace Mugabe katika mkutano wa makanisa iliyopangwa na African National Union- Patriotic Front (Zanu PF) Harare tarehe 5 Novemba. Haki miliki ya picha AFP

Siku ya Jumapili, wakazi wa Zimbabwe wanacheza ngoma katika mkutano wa injili ulitumika kama mkutano wa siasa iliyofanyika mjini Harare...

Wakristo nchini Zimbabwe kutoka kanisa tofauti wanamskiza bibi ya Rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe akihotubia mkutano mjini Harare tarehe 5, Novemba. Haki miliki ya picha AFP

Wengi wa waliohudhuria walikuwa wakristo wa tabaka mbali mbali...

Wafuasi wa Rais wa Zimbabwe wanakusanyika katika majengo kuu ya chama chake kumuunga mkono Grace Mugabe kuwa naibu wa rais mtarajiwa baada ya kufuutwa kazi kwa Emerson Mnangagwa Novemba 8 2017 Haki miliki ya picha AFP

Mrengo wa vijana wa chama tawala Zanu-PF nao walipanga mkusanyiko huu ili kuonyesha uaminifu wao kwa mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe...

Rais Mugabe amskiza bibiye Grace Mugabe katika mkutano wa siasa wa chama chake cha ZANU-PF mjini Harare, Zimbabwe, Novemba 8,2017 Haki miliki ya picha AFP

Alikuwepo na mumewe mwenye miaka 93, Rais Robert Mugabe. Bi Mugabe alitoa hotuba kali huku akionekana kuendeleza juhudi za kutaka kuchukua usukani kutoka kwa mumewe.

Moustafa, 15, abeba fani za uzi mjini Cairo, Misri, 07 Novemba 2017.Uzi hii inatumiwa kutengeneza nyuzi za viatu na godoro. Haki miliki ya picha EPA

Jumanne, Moustafa, 15, anabeba nyuzi katika kiwanda kilichosalia pekee katika eneo nzee la mji wa Cairo, Misri...

Salama, 76, mmiliki wa kiwanda hiki alianza kufanya kazi hii akiwa miaka 7 wakati wa utawala wa mfalme Farouk aliyesemekana kuwashika wanaume wote ambao hawakuwa wanafanya kazi.

Sasa zaidi ya miaka 70 baadaye kiwanda hiki ndicho kimesalia pekee eneo la kale la Cairo. Nyuzi hizi hutumiwa kutengeneza kamba za viatu na migodoro.

Salama, 76, mmiliki wa kiwanda hiki alianza kufanya kazi hii akiwa miaka 7 wakati wa utawala wa mfal,e Farouk aliyesemekana kuwashika wanaume wote ambao hawakuwa wanafanya kazi. Sasa zaidi ya miaka 70 baadaye kiwanda hiki ndiyo imesalia pekee eneo nzee la Cairo. Uzi hii inatumiwa kutengeneza nyuzi za viatu na godoro. Haki miliki ya picha EPA

Salama, 76, mmiliki wa kiwanda hiki alianza kufanya kazi hii akiwa miaka 7.

Wavuvi nchini Libya wanatia nanga katika bandari ya Tripoli, Novemba 3, 2017. Haki miliki ya picha EPA

Wavuvi nchini Libya wanatia nanga katika bandari ya Tripoli, Novemba 3, 2017.

Samaki zauzwa katika soko la samaki mjini Tripoli, Libya Novemba 3, 2017 Haki miliki ya picha Reuters

Samaki wauzwa katika soko la samaki mjini Tripoli, Libya Novemba 3, 2017

Picha hii ilipigwa Alhamisi, tapureta iliyo katika maonyesho yaliyofanyika katika jumba la makumbusho la polisi mjini Cape Town, Afrika Kusini. Haki miliki ya picha EPA

Picha hii ilipigwa Alhamisi, taipureta iliyo katika maonyesho yaliyofanyika katika jumba la makumbusho la polisi mjini Cape Town, Afrika Kusini.

Jumba hili la makumbusho pia inaonyesha mfano wa jinsi maafisa walivyokuwa karne ya 1913-1957. Haki miliki ya picha EPA

Jumba hili la makumbusho pia linaonyesha mfano wa jinsi maafisa walivyokuwa karne ya 1913-1957.

Images courtesy of AFP, EPA, PA and Reuters

Mada zinazohusiana