Mshukiwa awazuia polisi kwa kujamba Kansas, Marekani

Sean Sykes Jnr mug shot Haki miliki ya picha jackson county detention center
Image caption Sean Sykes Jnr, 24, alifanya mambo kuwa magumu kwa makachero

Mahojiano ya polisi na mshukiwa katika mji wa Kansas, Missouri nchini Marekani yalisitishwa ghafla baada ya mshukiwa huyo kujibu maswali ya polisi kwa kutoa ushuzi kwenye tupu yake ya nyuma.

Taarifa katika vyombo vya habari huko zinasema Sean Sykes Jnr alikuwa anakabiliwa na makosa ya kumiliki bunduki kinyume cha sheria na pia kuwa na dawa za kulevya.

Alikuwa amesimamishwa na polisi akiendesha gari mara mbili mjini Kansas.

Aliachiliwa awali Septemba lakini akazuiliwa tena mwezi huu.

Maelezo sasa yametolewa kuhusu jinsi mahojiano ya mwanzo ya Sykes na polisi yalivyositishwa ghafla Septemba.

Kwa mujibu wa gazeti la Kansas City, ripoti ya kachero aliyekuwa akimhoji inasema Sykes "aliinama upande mmoja wa kiti na kujamba kwa nguvu" alipoulizwa na polisi anwani yake wakati wa mahojiano Septemba.

Malawi kupiga marufuku

"Sykes aliendelea kushuta na hivyo tukasitisha mahojiano," kachero huyo aliandika, baada ya kupata nafuu.

Hakuna mashtaka yoyote yaliyokuwa yamewasilishwa dhidi ya Bw Sykes baada yake kukanusha kwua na ufahamu wowote kuhusu vitu alivyodaiwa kukamatwa navyo.

Lakini mwanamume huyo wa miaka 24 alisimamishwa tena na polisi mwezi huu. Ameshtakiwa kuwa na bunduki iliyokuwa imeibiwa na kuwa na nia ya kuuza kokeni.

Ripoti hiyo ya kachero ilifichuliwa mshukiwa alipofikishwa kortini Jumatatu.


Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii