Ndovu afanyiwa upasuaji kwenye pembe Colombia

Tantor the Elephant at Barranquilla Zoo has surgery 11/11/17 Haki miliki ya picha Jorge_Chavez
Image caption Ndovu afanyiwa upasuaji kwenye pembe Colombia

Hifadhi moja wa wanyama nchini Colombia umemfanyia upasuaji ndovu mmoja wa uzito wa tani tano aliyepatikana katika shamba moja linalomilikiwa na walanguzi wa madawa ya kulevya.

Wati 30 walishiriki wakati ndovu huyo kwa jina Tantor alidugwa dawa ya kumpa usingizi.

Upasuaji ulifanywa kwa pembe yake iliyokuwa imepasuka.

Zaidi ya watu 100 walichanga pesa kwa upasuaji huo ambao uligharimu zaidi ya dola 8,500.

Haki miliki ya picha Jorge_Chavez
Image caption Ndovu afanyiwa upasuaji kwenye pembe Colombia

Upasuaji huo ungefanyika miaka miwila iliyopita wakati Tantor alijeruhi pembe yake, likini shughuli hiyo ilichelewa baada ya kukosekana kwa vifaa vinavyostahili ili kufanya upasuaji.

Iibidi vifaa maalumu kutengenezwa kwa upasuaji huo.

Tantor alipekwa katika hifadhi ya Barranquilla Aprili mwaka 1991 wakati alipatwa na shirika la kupambana na madawa ya kulevya nchini Colombia kwenye shamba moja linalomilikiwa na walanguzi wa madawa ya kulevya.

Anaaminiwa kuwa na umri wa karibu miaka 50.

Mada zinazohusiana