Mwanajeshi wa Korea Kaskazini aliyehamia K Kusini alipigwa risasi 5

Mwanajeshi wa Korea kaskazini aliyehamia K Kusini alipigwa risasi 5 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwanajeshi wa Korea kaskazini aliyehamia K Kusini alipigwa risasi 5

Mwanajeshi wa Korea Kaskazini aliyeasi na kuvuka katika eneo la ulinzi mkali alipigwa risasi mara tano na sasa yuko katika hali maututi, Korea Kusini imesema.

Mwanajeshi huyo alivuka kuelekea upande wa kusini mwa Korea kusini upande wa eneo lenye ulinzi mkali ( JSA) katika kijiji cha Panmunjom siku ya Jumatatu.

Alikuwa amepeleka gari karibu na eneo la hilo la JSA, lakini ilibidi akamilishe safari kwa mguu wakati gurudumu la gari lake lilipolegea , Korea Kusini imesema.

Wanajeshi wa Korea Kaskazini walimmiminia risasi mara 40 lakini bado alifanikiwa kuvuka na akapatikana chini ya majani ya miti, iliongezea.

Takriban watu 1,000 kutoka Kaskazini huamia kusini kila mwaka lakini watu wachache uhamia kupitia eneo hilo lenye ulinzi mkali la (DMZ) ambapo ni mojawepo ya eneo lenye ulinzi mkali ulimwenguni.

Pia si kawaida kwa raia wa Korea Kaskazini kuvuka eneo la JSA , ambalo ni kivutio cha watalii na eneo pekee ambapo DMZ na vikosi vyote huonana ana kwa ana.

Korea Kaskazin na Korea Kusini wako bado vitani , tangu vita kati yao vilivyokamilika 1953 baada ya makubaliano na sio kwa kutia saini mkataba wa amani.

Mada zinazohusiana