Uchunguzi wa ini kuwasaidia wanaotumia madawa kupita kiasi

Paracetamol
Image caption Uchunguzi wa ini kuwasaidia wanaotumia madawa kupita kiasi

Watu ambao hutumia dawa za kupunguza maumivu za paracetamol kupita kiasi wanaweza kusaidiwa na uchunguzI wa damu papo hapo iwapo wataugua ugonjwa wa ini.

Watafiti waliofanya uchunguzi huo huko Edimburgh na Liverpool wamesema itaweza kuwasaidia madaktari kubaini mgonjwa anapowasili hospitalini iwapo anahitaji matibabu zaidi.

Uchunguzi wa damu hubaini kiwango cha chembechembe kwenye damu zinazohusiana na uharibifu wa ini.

Uchunguzi wa hapo awali umeonyesha kiwango cha dalili hizo huongezeka kwa wagonjwa ambao wanaugua ugonjwa wa ini kabla uchunguzi kamili kubanishwa.

Watafiti hao wamebaini utafiti huo unauwezo wakutabiri mgonjwa gani atapatwa na shida za ini na ambao wanaohitaji matibabu ya muda mrefu kabla ya kutolewa hospitalini.

Uchunguzi huo pia utasaidia wagonjwa ambao huweza kupokea matibabu na kwenda nyumbani.

Watu wengi hutumia dawa hiyo ya kupunguza maumivu ya paracetamol kupita kiasi hasa wakati wa kupokea tiba ya homa, ambazo pia dawa hizo huwa na kiungo flani cha paracetamol.

Uharibifu wa ini ni tatizo ambalo husababishwa na matumizi ya dawa kupita kiasi.Wakati wengine humuathiri mgonjwa na hata husababishia mgonjwa kufanyiwa upasuaji na kubadilishwa ini na pia huwa hatari kabisa.

Wagonjwa ambao wako katika hali mbaya kwa kutumia kiwango kikubwa cha paracetamol kwenye damu inaweza kutibiwa na dawa kwa jina acetylcysteine inapitishwa kupitia mishipa.

Matibabu hayo yanahusishwa na matatizo mengine kwa hivyo madaktari hawawatibu wagonjwa kwa muda mrefu.

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea