Maelfu ya watu wapo kwenye uhitaji Iran baada ya kupigwa na kimbunga

Watu wakiwa nje ya nyumba zao zilizoharibiwa vibaya
Image caption Watu wakiwa nje ya nyumba zao zilizoharibiwa vibaya

Baada ya saa saa 48 tokea kimbunga kikali kuupiga mpaka wa Iraq na Iran, maelfu ya watu bado wapo kwenye uhitaji mkubwa wa vitu muhimu.

Uharibifu mkubwa umetokea kwa upande wa Iran na majeruhi wanalalamikia zoezi la uokoaji kuwa haliridhishi.

Wengi wapo nje kwa siku ya tatu bila msaada wowote.

Zaidi ya watu 460 walikufa katika tetemeko hilo huku maelfu wakijeruhiwa vibaya.