Magufuli aagiza kubomolewa kwa jengo la shirika la kuzalisha Umeme, Tanesco.

Haki miliki ya picha TANESCO
Image caption Makao makuu ya shirika la kuzalisha na kusambaza umeme, TANESCO

Katika ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara katika eneo la Ubungo mjini Dar es salaam,Rais Magufuli ameagiza sehemu ya jengo ambalo ni makao makuu ya shirika linalozalisha na kusambaza umeme, TANESCO, kuwekwa alama ya 'X' kuashiria jengo hilo libomelewe.

Jengo jingine ambalo litaathiriwa na agizo hilo ni jengo la wizara ya maji ambalo lipo jirani.

Imeagizwa majengo hayo kubomolewa kutokana na kuwa yamejengwa katika sehemu ya hifadhi ya barabara.

Zoezi la bomoa boma limekuwa likiendelea, ambapo majengo pembezoni ya barabara inayounganisha mji wa Dar es salaam na maeneo mengine ya nchi yameathirika. Wakaazi wengi waliokuwa wakiishi katika maeneo yanayodaiwa kuwa katika hifadhi ya barabara wamepoteza makazi yao.

Mada zinazohusiana