Ufaransa yamualika waziri mkuu wa Lebanon Saad Hariri

Posters depicting Saad Hariri seen in Beirut, Lebanon, November 14, 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mabango ya Saad Hariri kwenye barabara za mji mkuu wa Lebanon, Beirut

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemualika waziri mkuu wa Lebanon Saad Hariri na familia yake kwenda Ufaransa lakini amesema kuwa hampi hifadhi ya kisiasa.

Maafisa wa Ufaransa wanasema kuwa Bw. Hariri atawasili siku chache zinazokuja.

Bw Hariri alijiuzulu ghafla wakati akiwa ziarani nchini Saudi Arabia tarehe 4 Novemba, na kuzua msuko suko wa kisiasa.

Serikali ya Saudi Arabia imekana kumzuilia bila ya mapenzi yake au kumlazimisha kujiuzulu katika jitihada za kukabiliana ushawishi wa hasimu wake Iran.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Saad Hariri na Emmanuel Macron walifanya mazungumzo mjini Paris September

Siku ya Jumatano rais wa Lebanon Michel Aoun aliilaumu Saudi Arabia kwa kumzui Bw Hariri akisema hakuna sababu ya yeye kutokuwepo Lebanon.

Hata hivyo Bw. Hariri amesisitzia kuwa yuko salama na karibuni atarudi Lebanon.

Bw. Macron akiongea wakati alifanya ziara nchini Lebanon alisema mwaliko huo wa kuzuru Ufaransa ulitolewa wakati alizungumza na Bw Hariri na mfame wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman kwa njia ya simu.

Alipoulizwa ikiwa anampa Bw Hariri hifadhi, alisema 'Hapana, Nina matumaini kuwa Lebanon itakuwa salama na kuwa hatua za kisiasa zitafanywa kisheria.

Mada zinazohusiana