Anawasaidia wanawake wanaowatoroka al-Shabab
Huwezi kusikiliza tena

Hamisa: Mwanamke anayewasaidia wanawake wanaowatoroka al-Shabab

Vijana wengi mjini Mombasa wanaotoroka kundi la Al Shabaab kutoka Somalia na kurudi pwani ya Kenya hujikuta hawana la kufanya kwani miongoni mwao watu wao na majirani huwatenga.

Lakini mama Hamisa Maalim Zaja ameamua kuwasaidia hasa wanawake kwa kuwaanzishia biashara mbali mbali.

John Nene amezungumza na Hamisa pamoja na wanawake wanaonufaika kwa mradi wake huo.

Mmoja wao alihadaiwa na ndoa kisha kufika Somalia akawa baadhi ya wanawake wanaowasaidia Al Shabaab na kazi za nyumbani lakini baada ya wiki mbili alipata mwanya na kutoroka pamoja na wenzake wawili

Mada zinazohusiana