Mwanajeshi wa zamani ashinda uchaguzi wa urais Somaliland

Muse Bihi Abdi aliibuka mshindi kwa kujipatia asilimia 50 ya kura hizo.
Image caption Muse Bihi Abdi aliibuka mshindi kwa kujipatia asilimia 50 ya kura hizo.

Mgombea wa chama tawala cha Kulmiye ameshinda uchaguzi wa urais katika eneo lililojitenga la Jamhuri ya Somaliland.

Mwanajeshi wa zamani Muse Bihi Abdi aliibuka mshindi kwa kujipatia asilimia 50 ya kura hizo.

Chama kikuu cha upinzani cha Wadani kimesema kuwa kulikuwa na udanganyifu wakati wa uchaguzi huo.

Watu kadhaa wameuawa kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi.

Bwana Bihi ni rais wa tano wa Somaliland tangu ilipojitenga na Somalia 1991.

Anakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo idadi kubwa ya watu wasio na ajira , kiangazi na kutotambuliwa kwa Somaliland.

Mada zinazohusiana