Rais Robert Mugabe amejiuzulu

Rais Robert Mugabe amejiuzulu
Image caption Rais Robert Mugabe amejiuzulu

Spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .

Spika wa bunge Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko ya amani ya mamlaka kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.

Haki miliki ya picha AFP/getty
Image caption Nukuu ya rais Mugabe alipokuwa akijiuzulu

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters, Spika wa bunge amesema kuwa kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya Jumatano.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raia wa Zimbabwe wafurahia kujiuzulu kwa Mugabe

Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.

Huwezi kusikiliza tena
Je,ni Kiongozi mkombozi ,mfisadi au mwonevu?

Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka mamlakani wiki hii.

Amekuwa mamlakani tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake 1980.

Bwana Mugabe ameshinda uchaguzi wa urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15 iliopita shughuli hiyo imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake.

Ameongoza kipindi cha uchumi ulioanguka ambapo raia wamezidi kuwa masiki zaidi ya walivyokuwa 1980.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raia wa Zimbabwe katikati ya mji mkuu wa Harare wakifurahia kuzjiuzulu kwa Mugabe

Hatua iliosababisha yeye kuanza kung'atuliwa madarakani ni ile alipomfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa wiki mbili zilizopita.

Hatua hiyo ilionekana na wengi kama ya kutaka mkewe kumrithi.

Iliwaudhi viongozi wa jeshi ambao waliingilia kati na kumweka rais Mugabe katika kizuizi cha nyumbani.

Huwezi kusikiliza tena
Ni Shangwe mjini Harare kufuatia kujiuzulu kwa Mugabe

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema kuwa kujiuzulu kwa Mugabe kunaipatia Zimbabwe fursa ya kuwa na mwanzo mpya kufuatia ukandamizaji uliotawala uongozi wa Mugabe.

Amesema kuwa Uingereza ambaye ni rafiki wa zamani wa Zimbabwe atafanya kila awezalo kusaidia kufanyika kwa uchaguzi ulio huru na haki na kujenga uchumi wa Zimbabwe.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Robert Mugabe ajiuzulu

Ubalozi wa Marekani mjini Harare umesema kuwa ni hatua ya kihistoria na kuwapongeza raia wa Zimbabwe kwa kutoa sauti zao na kusema kwa njia ya amani kwamba ni wakati wa mabadiliko.

Chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance kilifurahia hatua hiyo kikisema kuwa bwana Mugabe alibadilika kutoka kuwa mkombozi hadi dikteta.

''Ninafuraha sana leo kwa sababu nimekuwa nikiamini kwamba Mugabe atajiuzulu katika maisha yangu na imefanyika'', alisema mwanaharakati wa haki za kibinaadamu Linda Masarira aliyekuwa akizungumza na BBC.

''Na sasa kwenda mbele ni wakati wa upinzani kujiandaa na kuona kwamba tunakuwa na serikali inayowajali raia wake.Na kila mtu lazima ashirikishwe''.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii