Mnangagwa aapa kuwahudumia raia wote wa Zimbabwe

Mnangagwa akichukua kiapo cha kuwa rais
Image caption Mnangagwa akichukua kiapo cha kuwa rais

Raia wa Zimbabwe wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa michezo mjini katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare kwa ajili ya sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa.

Mnangagwa ameapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla.

Emmerson Mnangagwa, kwa jina la utani The the crocodile", ameanza hotuba yake kama rais wa Zimbabwe.

''Nahisi furaha sana kwa uamuzi wa chama cha Zanu PF kunialika kuhudumia taifa letu la Zimbabwe kama rais na kamanda mkuu wa majeshi kuanzia leo''.

''Sina ujuzi wa kazi hii lakini nitawahudumia wananchi wote bila upendeleo wa rangi ama kabil''a. Amemsifu Robert Mugabe kwa kupiginia uhuru huku akisema kuwa alichukua uongozi wakati mgumu .

Amesema kuwa licha ya makosa yaliofanywa na Mugabe ni muhimu kukubali na kutambua mchango wake kuhusu ujenzi wa taifa. ''Kwangu mie bado ni rafiki mkubwa''.

amesema kuwa jukumu lake halitatekelezwa kupitia hutuba.

Image caption Raia wakimshangilia rais Mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa
Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Wafuasi wa rais mpya wa Zimbabwe

Lazima nianze kazi....

Tutaanza kazi kwa haraka kutoka pale alipowachia aliyekuwa rais wetu Robert Mugabe.

Hatuwezi kubadili yaliopita, kuna mengi ambayo tunaweza kufanya kwa sasa ili kulipatia taifa letu mwelekeo mpya.

Hatuwezi kukubali kuwa watumwa wa yaliopita.

Amesema kuwa mabadiliko ya umiliki wa ardhi yalifanyika na hayawezi kubadilishwa kwa kuwa huo utakuwa ukiukaji mkuu wa upiganiaji wa Uhuru.

Lakini rais huo mpya ameahidi kuwalipa wakulima waliopoteza mashamba yao katika sera tata iliotekelezwa na utawala wa rais MUgabe.

Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano -ameapishwa katika uwanja michezo wa Harare.

Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke .

Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza "utamaduni wa ufisadi". Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 hapo siku ya Jumanne iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe.

Haki miliki ya picha Twitter /Caesarzvai
Image caption Raia wa Zimbabwe akiwa amevalia kiatu cha muundo wa mamba, kama ishara ya kumuunga mkono rais mpya Emmerson Mnangagwa anayejiita ''Mamba''.

Ilitolewa kwa njia ya barua bungeni na kikao cha kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae kikakatizwa.

Katika barua hiyo Bwana Mugabe alisema anajiuzulu ili kuruhusu mchakato rahisi na wa amani wa ukabidhianaji mamlaka na kwamba uamuzi wake ulikuwa wa hiari.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Mugabe alishutumiwa kwa kumuandaa mkewe Grace kuchukua wadhfa wa urais

Bwana Mugabe na mkewe Grace hawajaonekana hadharani tangu Jumapili, na haifahamiki wako wapi .

Alhamis , taarifa zilielezea kuwa Bwana Mugabe amepewa kinga ya kutoshtakiwa.

Televisheni ya taifa imesema kuwa atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Bwana Munangagwa.

Sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa michezo mjini Harare wenye viti 60,000- huku waandalizi wakiwataka waZimbabwe kuhudhuria kwa wingi sherehe hizo.

lhamisi Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini (MDC ) alitoa wito wa kufanyika kwa mageuzi makubwa ya kisiasa ili kuondoa masuala yaliyoweka madarakani kwa muda mrefu utawala wa Bwana.

Image caption Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement fo Democratic Change (MDC) Morgan Tsvangirai

Bwana Munangagwa alikimbilia nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita- na kurejea nchini Jumatano wiki hii ambapo alipokelewa kama shujaa.

Bwana Mnangagwa aliahidi kubuni ajira ambapo baadhi wanakadiria kuwa 90% ya watu hawana ajira.

"Tunataka kukuza uchumi wetu, tunataka amani, tunataka kazi, kazi, kazi ," aliuambia umati wa watu uliomshangilia mjini Harare.

Jumatano chama tawala cha ZANU PF kilisema kitafanya mageuzi kuondoa sheria zilizomfanya Mugabe kuwepo madarakani kwa muda mrefu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii