Odinga asema naye ataapishwa kuiongoza Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Odinga asema naye ataapishwa kuiongoza Kenya

Kiongozi wa muungano wa upinzani Kenya wa National Super Alliance Raila Odinga amesema kuwa naye pia ataapishwa kuiongoza Kenya.

Amesisitiza kwamba hamtambui Bw Kenyatta kama rais wa Kenya.

Akihutubia wafuasi wake karibu na uwanja wa Jacaranda ambapo upinzani ulizuiwa kuandaa mkutano, amesema ataapishwa na mabaraza ya wananchi tarehe 12 Desemba.