Wakuu wa jeshi wateuliwa kuwa mawaziri Zimbabwe

Rais Emmerson Mnangagwa amewateua wakuu wa jeshi katika baraza lake jipya la mawaziri
Image caption Rais Emmerson Mnangagwa amewateua wakuu wa jeshi katika baraza lake jipya la mawaziri

Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amelitaja baraza lake la mawaziri akimteua afisa mkuu wa jeshi kwa wadhfu mkuu katika serikali yake.

Waziri mpya wa fedha ni Sibusiso Moyo , jenerali aliyetangaza katika runinga ya taifa hilo wiki mbili zilizopita kwamba jeshi limechukua udhibiti.

Mkuu wa jeshi la angani Perence Shiri ataongoza wizara ya fedha na kilimo.

Kiongozi mmoja wa upinzani Tendai Biti amesema kuwa fungate iliokuwa ikisherehekewa Zimbabwe imeisha kabla ya kuanza.

Bwana Mnangagwa aliapishwa wiki moja iliopita kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe ambaye alikuwa mamlakani kwa takriban miaka saba.

Upinzani umelaumu mabadiliko hayo kama usaliti wa matumaini miongoni mwa raia na thibitisho kuwa vikosi vya usalama vilivyokuwa na nguvu nyingi wakati wa utawala wa Mugabe vinaendelea kuthibiti taifa hilo.

Hali ya kuleta uwiano na umoja ilioonekana katika siku za karibuni huenda ikabadilishwa na makabiliano ya uongozi katika uchaguzi wa mwaka ujao.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii