Trump kutambua Jerusalem ni mji mkuu wa Israel

Donald Trump kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel
Image caption Donald Trump kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel

Maafisa nchini Marekani wanasema kuwa Rais Trump anatarajiwa kutangaza wiki ijayo kuwa Marekani inatambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel hatua ambayo wakosoaji wanasema kuwa itachochea mzozo zaidi katika eneo hilo.

Hali kamili ya mji huo inakumbwa na utata huku pande zote mbili za Israel na Palestina zikidai kuwa ndio mji wao mkuu.

Trump alitoa ahadi ya kampeni ya kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem.

Image caption Mji wa Jerusalem

Mwandishi wa BBC anasema kwa kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, Trump anaashiria hatua ya kutekeleza ahadi yake ya kampeni.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii